*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*
*NENO KUU.*
TRH. 18/06/2021.
MCH. MARK. WALWA MALEKANA.
*SOMO: SIKU YA KUMBUKIZI LA UUMBAJI.*
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:28
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:29
Katika maisha haya kuna makumbukizi ya aina mbalimbali kama vile siku ya kuzaliwa, au ya uhuru na matukio mbalimbali. Lakini Mungu anayo siku ya pekee ya Kumbukizi duniani mwote.
Baada ya Uumbaji Mungu aliweka siku ya pekee iwe kumbukizi nayo ni SABATO.
Biblia inamsemaje au inamtambulishaje Mungu?
Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu.
Isaya 40:25
Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
Isaya 40:26
Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
Isaya 40:28
Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.
Isaya 41:4
Mungu Bwana anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
Isaya 42:5
Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;
Isaya 42:6
kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Isaya 42:7
Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Isaya 42:8
Mungu ni Muumbaji wa malimwengu wote. Wa Kwanza na wa Mwisho.
Ni makosa makubwa kutengeneza kinyago ukikiita Mungu, MUNGU ni Muumbaji ni Mkuu wa mataifa yote hafananishwi na chochote kile.
Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru.
Isaya 45:12
Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?
Isaya 40:18
Sanamu fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha.
Isaya 40:19
Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
Isaya 40:20
Mungu ni Mkuu, Muumbaji na Mruzuku. Hakuna wa kufanana naye.
Mungu aliweka mhuri wa siku ya pekee ili kukumbuka kazi yake ya Uumbaji.
Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Mwanzo 2:1
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
Mwanzo 2:2
Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Mwanzo 2:3
Katika Siku ya sabato Mungu Alipumzika, Aliibariki, na Akaitakasa.
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Kutoka 20:8
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
Kutoka 20:9
lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Kutoka 20:10
Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Kutoka 20:11
Kwanini "Ikumbuke?" Ili kuweka katika uzito na maanani(Keep into Consideration)
Mwanadamu ni lazima atende kazi na siku ya Sabato apumzike.
Neno Sabato maana yake ni Pumziko(Rest). Yaani kukoma kufanya kitu fulani.
Kwanini Sabato.
Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.
Ezekieli 20:12
Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.
Marko 2:27
Nani Mwenye Sabato?
Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;
Isaya 58:13
ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.
Isaya 58:14
Sabato ni kumbukumbu ya Wokovu.
Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake.
Zaburi 105:42
Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.
Zaburi 105:43
Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu;
Zaburi 105:44
Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.
Zaburi 105:45
Mfalme wa Misri akawaambia Enyi Musa na Haruni, mbona mnawaachisha watu kazi zao? Enendeni zenu kwa mizigo yenu.
Kutoka 5:4
Kisha Farao akasema, Tazameni, watu wa nchi sasa ni wengi, nanyi mnawapumzisha, wasichukue mizigo yao.
Kutoka 5:5
Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru.
Kumbukumbu la Torati 5:12
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
Kumbukumbu la Torati 5:13
Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
Kumbukumbu la Torati 5:15
Yesu alitunza Sabato pia.
Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
Luka 4:16
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.
Luka 23:54
Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa.
Luka 23:55
Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.
Luka 23:56
Mitume walitunza Sabato? Ndiyo.
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
Matendo ya Mitume 17:2
Mungu anasemaje kwa watu wake wa mwisho?
Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
Isaya 56:6
Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Isaya 56:7
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
Isaya 66:23
UJUMBE WA MUNGU KWETU LEO NI HUU;
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
Ufunuo wa Yohana 14:6
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Ufunuo wa Yohana 14:7
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
chirongemagai74@gmail.com
🙏🙏🙏🙏
0 Comments