*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*
NENO KUU.
TRH. 17/06/2021.
MCH. MARK. WALWA MALEKANA.
*SOMO: SHERIA BORA ZAIDI DUNIANI.*
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:28
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:29
Ulimwengu unatawaliwa na sheria ili watu waongozwe kwazo. Sheria za mataifa mbalimbali ulimwenguni zimekuwepo kadha wa kadha. Lakini wakati mwingine zilikuwa kali mno yaani ni sheria za jino kwa jino. Kwa ujumla ni kwamba sheria za ulimwengu zina upungufu ndiyo maana wakati mwingine hufanyiwa mabadiliko au marekebisho, hivyo leo tuaangalia sheria bora zaidi duniani ambayo ni sheria ya Mungu milele zote na haibadiliki kamwe. Je, ni sheria gani hiyo?
Sheria ilitoka wapi? Nani ameanzisha sheria? Vitabu vitano vya Musa hujulikana kama vitabu vya sheria. Leo tunazungumzia kiini cha sheria ya serikali ya Mungu. Hii ni sheria aliyoihubiri Mungu mwenyewe katika mlima wa Sinai kupitia Kiongozi Musa.
Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.
Matendo ya Mitume 7:22. Musa alisomea maswala ya Sheria, Muziki, Jeshi.
Basi, Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake; mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa.
Kutoka 32:15
Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao.
Kutoka 32:16
Sheria hii imeandikwa na Mungu mwenyewe kwa mikono yake.
Musa aliambiwa hivi na Mungu;
Kisha Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, hizo ulizozivunja.
Kutoka 34:1
Nawe uwe tayari asubuhi, na asubuhi ukwee juu katika mlima wa Sinai, nawe hudhurisha nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima.
Kutoka 34:2
Wakati ule Bwana akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti.
Kumbukumbu la Torati 10:1
Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku.
Kumbukumbu la Torati 10:2
Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu.
Kumbukumbu la Torati 10:3
Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia Bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; Bwana akanipa.
Kumbukumbu la Torati 10:4
Amri kumi ziliandikwa kwa kidole cha Mungu mwenyewe. Ziliandikwa katika mawe ili ziwe ishara ya milele zote yaani haziwezi kufutika. Hii ndiyo sheria bora kuliko zote(Amri kumi za Mungu) ni ya watu wote.
Sheria inakutaka ufe lakini juu ya sheria kuna Neema ya Mungu, kwa wale wanaompokea na kumwamini kikamilifu.
Hadhi ya sheria ni ipi? Ni takatifu, ya haki na njema
Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.
Warumi 7:12
Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.
Zaburi 19:7
Kudumu kwa amri kumi, hizi ni za kudumu milele zote.
Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe.
Kumbukumbu la Torati 4:13
Sheria haibadiliki kama Mungu asivyobadilika.
Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
Malaki 3:6
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Mathayo 5:17
Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
Mathayo 5:18
Sheria ya Mungu haikosei wala haibadiliki milele zote.
Msingi wa sheria ni nini hasa? Ni UPENDO KWA MUNGU NA KWA MWANADAMU.
Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
Mathayo 22:36
Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Mathayo 22:37
Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
Mathayo 22:38
Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Mathayo 22:39
Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Mathayo 22:40
Upendo kwa Mungu na upendo kwa mwanadamu mwenzako.
Je, Mungu alifuta amri? Hapana.
Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Warumi 13:8
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Warumi 13:9
Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
Warumi 13:10
Ukimpenda jirani yako utamheshimu siku zote hutazini naye wala kumwibia.
Kazi ya sheria ni nini? Kutuonyesha dhambi zetu.
kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Warumi 3:20
Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
1 Yohana 3:4
Wengi hawapendi sheria kwakuwa zinafunua jinsi walivyo yaani tabia zao mbaya.
Kazi nyingine, sheria ni kipimo cha hukumu pia.
Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
Yakobo 2:12
Ni ushahidi tosha kuwa uko ndani ya Mungu.
Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
1 Yohana 5:2
Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
1 Yohana 5:3
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
1 Yohana 3:9
Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
1 Yohana 2:4
Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
1 Yohana 2:5
Yesu mwenyewe anasema,
Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Yohana 14:15
Ahadi ya Mungu kwa siku za mwisho ni hii:
Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.
Zaburi 119:97
Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote.
Zaburi 119:98
Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
Zaburi 119:99
Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
Zaburi 119:100
Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;
Waebrania 8:8
Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
Waebrania 8:10
Amri za Mungu ziko katika kitabu cha Kutoka 20:1-17.
Hakuna aliye huru pasipo kushika na kutunza amri za Mungu.
*MUNGU ATUBARIKI SOTE TUNAPOAMUA KUTUNZA SHERIA ZAKE KIKAMILIFU MIOYONI MWETU.*
chirongemagai74@gmail.com
🙏🙏🙏🙏
0 Comments