*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*
KAYA NA FAMILIA.
TRH. 17/06/2021.
DEVOTHA SHIMBE.
*SOMO: MAWASILIANO KATIKA NDOA.*
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Yakobo 1:19
kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
Yakobo 1:20
Mawasiliano ni kutoa na kupokea taarifa na kuielewa inavyopaswa.
Njia za mawasiliano hutegemea mwonekano wa uso, matendo yako, ishara na hisia zako wakati unapoongea.
Kanuni tatu za mawasiliano.
1. Huleta uhai ikiwa yatazingatia sanaa za kuzungumza.
2. Huleta shangwe kwa njia ya kujenga na si kubomoa.
3. Huleta ukaribu ikiwa yatatumika kwa kuambizana juu ya upendo na maneno ya kupenda hapo nyumbani. Mfano maneno kama vile nakupenda. Siku isipite hujamwambia neno la kujenga upendo katika ndoa mwenzi wako. Tafuta jina zuri la kumwita mwenzi wako.
Vizuizi katika mawasiliano:
1. Maneno ya bubabe au kushurutisha. Haya hayajengi ndoa kabisa.
2. Maonyo na vitisho.
3. Ukosoaji, lawama, kejeli, dharau. Hivi hubomoa familia na kuvunja hisia. Hufanya mwenzi wako kuwa duni wakati wako.
Vizuizi vya kusikiliza:
1. Mzungumzaji mchovu, yeye anajua kabla hujazungumza.
2. Msikilizaji mwenye kuchagua. Yaani hupenda mambo yanayowavutia tu basi, mengine hawazingatii kabisa. Sikiliza tu hata kama kinauma.
3. Msikilizaji mwenye kujilinda. Hubadili maneno yote ili kujilinda yeye.
4. Msikilizaji mkatizaji. Yeye hutafuta jibu na siyo kusikiliza.
5. Msikilizaji asiye na hisia. Hasomi hisia zako hata kama ni kusikitika yeye wala hajali. Unaongea kwa upole yeye anajibu kwa ukali bila kujali kabisa.
Tofauti ya kusikiliza kwa wanaume na wanawake:
Mara nyingi hujifanya kama hawasikii lakini wanawake hutumia ishara kama kutikisa kichwa.
Wanaume hukaza macho, wanawake hukazia macho wanaume.
Wanaume huingilia mazungumzo kwa kuingilia maswali. Lakini wanawake husubiri ili aweza kuuliza swali.
Tofauti za kuongea:
Wanawake huzungumza sana wanaume huzungumza kidogo.
Wanawake hutumia ubongo wa kulia wanawake hutumia ubongo wa kushoto.
Wanawake hutumia maneno ya wingi. Mwanaume maneno ya umoja.
Wanaume huficha hisia zao wanawake hawafichi hisia zao.
Nini kifanyike?
Mtazame mzungumzaji usoni.
Chagua muda sahihi wa kuzungumza.
Sikiliza sana kuliko kuongea sana.
Uwe muwazi na mkweli na ubaki kwenye mada.
Hakikisha unafanya mazungumzo ya kujenga siyo kubomoa.
Mtegemee Mungu naye hatawaacha kamwe.
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏
0 Comments