Advertisement

Responsive Advertisement

MWINYI AITAKA QATAR KUWEKEZA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiomba Serikali ya Qatar kuwashajihisha Wawekezaji wa nchi hiyo kuja nchini kuwekeza katika sekta za Utalii, Uvuvi pamoja na mafuta na Gesi.

Dk. Mwinyi ametoa ombi hilo Ikulu jijini Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Hussain Ahmad Al Humaid, aliefika kujitambulisha.

Amesema tayari Zanzibar imeanzisha Sera maalum kwa ajili ya kuendeleza Uwekezaji, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wake.

Rais Dk. Mwinyi aliiomba nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kuisaidia Zanzibar katika uimarishaji wa sekta za Maji, Afya pamoja na elimu.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili hizo, na kubainisha umuhimu wa hatua hiyo kuendelezwa katika sekta binafsi.

Aidha, Dk. Mwinyi alisema kuwepo kwa safari za Ndege kati ya Zanzibar na Qatar ni fursa muhimu ya kuendeleza biashara kati ya nchi mbili hizo, na kuiomba Qatar kuweka mazingira bora ya soko la bidhaa mbali mbali.

Post a Comment

0 Comments