Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na zoezi la utoaji wa elimu ya mwongozo wa kushughulikia malalamiko wakati wa utekelezaji wa miradi ya usafi wa Mazingira ambapo itahusisha ujenzi wa vyoo vya kisasa katika mtaa wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Utekelezaji wa miradi ya Usafi wa Mazingira utafanyika katika Wilaya zote tano za jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi Benki ya Dunia wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (WSSP II).
0 Comments