MCHANGO WA FAMILIA NA DINI KATIKA JAMII
*FIKIRI-TANK*:Kanisa la Efeso[31-100 A.D] Ufu 2:1-7
Sifa kubwa ya kanisa la Efeso ni upendo kupoa. Ni kanisa ambali limepoteza upendo wake wa kwanza.
*Muktadha* Neno "efeso" humaanisha *enye kutamanisha/vutia*. Efeso ulimkuwa mji muhimu sana katika koloni la Kirumi huko Asia. Katika koloni hili mji mkuu ulikuwa Pergamum. Jiji la Efeso lilikuwa lina bandari nzuri na lilikuwa kituo imara cha biashara. Mji huu uliheshimika kama kituo kikubwa cha dini za kipagani. Artemis/ Diana mungu mke wa uzao alikuwa akiabudiwa hapa , sanamu ya mungu huyu ilikuwa imejaa matiti mwili mzima. Hekalu la mungu huyu lilikuwa ni miongoni mwa maajabu 7 ya ulimwengu .
Wenzi katika utume: Kanisa la Efeso lilianzishwa na wanandoa wachamungu Aquila na Priscilla. Wainjilisti Apolo na Paulo walisaidia katika uanzilishi huu.[Mdo 18:18-26]. Paulo aliishi na kufanya kazi hapo Efeso kwa miaka mitatu.[Mdo 19:23-41];
Wanikolai ni watu gani?
Ni wakristo waliodhani Kristo amewaweka huru na utii wa amri 10. Walikuwa wakifanya uasherati na kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu ya sanamu.
JADILI
a/ *Moja ya kusudi la msingi kabisa la ndoa ni KUONGOA ROHO.* Unafikiri nini kuhusu sentensi hii?
b/ Ni kwa namna gani familia ya Aquila&Priscilla imechallenge mahusiano yako ya sasa? Je, mahusiano yako na mwenzio yanaisaidiaje jamii , marafiki au kanisa?
c/Mahusiano yako ni mfano kwa wengine kiasi gani? je, yakusanya pamoja na Kristo au Yanatapanya?
d/Unawashaurije watu *waliopitiliza* katika shughuli za kidini kiasi cha *kupuuzia* familia zao?
*PMC 360:2021*
Share kwa watu hapa chini,nao wajifunze ⏬
Post a Comment