MAZUNGUMZO YA HAKI NA YA WAZI YAFANYIKE
Serikali imewataka waajiri nchini kuruhusu vikao vya wanachama na vyama vya wafanyakazi na majadiliano kati ya waajiri na vyama vya wafanyakazi nchini ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi vinaboreshwa na tija ya kazi inaonekana.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Tixon Nzunda , alipofunga Semina ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) mjini Morogoro.
“Nitoe rai kwa waajiri na wasimamizi wa kazi kuhakikisha vikao vya wanachama na vyama vya wafanyakazi vinafanyika na mazungumzo ya haki na ya wazi yanafanyika kati ya waajiri na vyama vya wafanyakazi kuanzia ngazi ya service point (eneo la huduma) mpaka ngazi ya taifa,” ameagiza Nzunda.
Pia, katika kuhakikisha tija ya kazi inaonekana, Nzunda amewaasa wajumbe wa Baraza Kuu la TUICO na vyama vingine vya wafanyakazi nchini kuwasisitiza wanachama kufanya kazi kwa weledi na uadilifu wakati changamoto zao zikiendelea kutatuliwa.
“Naomba mpeleke meseji kwa wanachama wetu, watekeleze wajibu wao kwa kufanya kazi vizuri kwa misingi ya weledi, uadilifu na kuwajibika kwa umma. Tukifanya hivi mimi nitakuwa mtetezi wa wanachama kuliko wenyewe mnavyowatetea,” amesema Nzunda.
Nzunda ametumia semina ya Wajumbe wa Baraza Kuu la TUICO kuvitaka vyama vingine vya wafanyakazi kuiga mfumo na utaratibu kama wa TUICO wa kuwajengea uwezo wanachama, wajumbe na watendaji wake ili kuboresha utumishi na utendaji wa vyama vyao.
“Nitumie fursa hii kuwaagiza vyama vingine vya wafanyakazi kuiga utamaduni na mfumo huu wa kuandaa programu ya kujenga uwezo kwa wanachama na watumishi, tukiwa tunajitambua vizuri zaidi, tunaelewa dira na dhima ya vyama vyetu, lakini pia tukiwa tunaelewa dhana ya utumishi miongoni mwetu,” ameongeza Nzunda.
Nzunda amewakumbusha wajumbe wa Baraza Kuu la TUICO kuwa uongozi ni utumishi na sio kuwa bosi. Amewahimiza kuzingatia suala la “customer care” akimaanisha huduma bora kwa wanachama.
Vile vile Nzunda amebainisha nia ya serikali kuendelea kushirikiana na vyama.

Post a Comment