MAREKANI,VATICAN,SABATO NA COVID 19
#GREEN #SABBATH NI SABATO ILE ILE YA MAZINGIRA AMBAYO NI SIKU YA #Jumapili ITAKAPOPITISHWA #KISHERIA.(sehemu ya 3)
NI siku nyingine tena Nawasalimu wana na binti za MUNGU kupitia jina la YESU 😅🙏🏻.
Karibuni katika somo tajwa hapo juu👆🏻👆🏻.
Wapendwa katika Jina la BWANA , tunaishi kipindi cha kuagana kabisa. Waovu na wema sasa tunapungiana mkono wa #kwaheri, japo hatuoni mikono hiyo ikiashiria hiyo hali, lakini kwa macho ya ufahamu wa kiroho na akili ya kiroho tunaona kwa imani kwamba Wanadamu makundi mawili #YanaaganaMILELE na hayataonana tena.
1Petro 4:7👇🏻👇🏻
Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia, Basi iweni na #Akili , mkeshe katika #Sala.
Mtume petro akiongozwa na Roho wa Mungu, alivuviwa ili kutuonya wakristo wa leo na kutuambia kuwa, #MwishoUMEKARIBIA, yatupasa kuwa na #Akili ya kiroho na tuwe watu wa #Maombi mengi.
Bwana anatuambia kuwa mwisho wa kila jambo umekaribia, Bwana anatutaka tuwe na akili ya kuzitambua nyakati hizi za hatari, tuwe na akili ya kutambua miaka ambayo Yesu anakaribia kuja. Huu siyo wakati wa kusikiliza mahubiri yanayochekesha kutoka katika mimbari zetu za makanisa ndani ya sda, hatuna mda wa kusikiliza hadithi na visa vya kutunga na shuhuda za uongo. Mda uliobaki ni mda wa kumrejea BWANA kwa mioyo yetu yote. Na mioyo yetu itaguswa kwa ndani kabisa pale tutapourejea ujumbe wetu wa malaika watatu. Unabii huu wa malaika watatu ndio utakaogusa mioyo iliyotanga mbali na itamrudia BWANA . Unabii unafufua hali ya kiroho, na asiyeutaka unabii kamwe siyo mwenzetu na hawezi kuokolewa. Unabii unaamsha fahamu za mwanadamu , unabii unasadikisha mioyo juu ya hatia iliyomo ndani ya moyo, unabii unawavuta watu kwa MUNGU , unabii unabomoa mioyo ya mawe, ukafiri na kutojali hufukuziwa mbali na mtu hujinyenyekeza kwa BWANA kutafuta rehema zake.
#Wacho👉🏻world Action on Climate &Health Organization 👉🏻Ni harakati za dunia nzima ambazo zimeanzishwa na vaticani zikaletwa marekani , zikaletwa hadi kwenye shirika la umoja wa mataifa, na kisha kuagizwa kwa serikali zte duniani. Mabadiliko ya tabia ya nchi sasa yanashika kasi katika mikutano mikubwa ya dunia , Janga la kutengeneza la covid19 pia linazidi kushika kasi katika mikutano ya dunia.
Majanga haya ni ya kiwerevu wa kishetani na ambayo yanashikiliwa na mkono wa Vatican ulionyooshwa kuelekea kwenye pumziko la kiulimwengu la jumapili kisheria, itakayolazimishwa duniani kote, marekani ikiwa ni mkono wa kuume wa Vatican katika kuyalazimisha mataifa yote na watu wote kuitii sauti ya Vatican .
Ufunuo 13:11-18
Marekani itayalazimisha mataifa yote kuutii utawala na maagizo ya papa wa vatican . Kuutii upapa ni kumtii shetani, kwani Vatican ndipo kilipo kiti cha enzi cha joka. Ufunuo 13:2.
Papa wa vatican alinukuliwa na gazeti la CNN 9April 2020, alisema👇🏻👇🏻
Janga la covid19 litakuwa ni jibu la mazingira(Climate change) kutokana na mgogoro wa tabia ya nchi.
Gazeti la National Catholic Register April 8, 2020 . Je Janga la covid19 ni pigo toka kwa Mungu??
Gazeti hilo linasema, Nusu ya wanadamu sasa wako chini ya kizuizi(lockdown), Je tumeshindwa kumuheshimu Bwana mara nyingi kwa kuitunza siku ya BWANA ?? Je, hatujaifanya jumapili kama siku nyingine za kawaida?? Kama wakati wa kwenda kufanya manunuzi, kukamilisha majukumu, na kutekeleza ajenda zetu binafsi?? Badala ya kutumia mda kuimarisha mahusiano yetu na YESU na kustarehe na familia na marafiki??
Katika agano la kale Mungu alisema yuda atatengwa utumwani kwa wakati sawa na sabato zote alizozivunja, hadi nchi itakaporejea katika sabato yake iliyopotea. 2Nyakati 36:21. Kwa hiyo jamii yetu inafidia sabato ilizozipoteza. #mwisho wa kumnukuu papa Francis.
👉🏻Huu ndo udanganyifu wa vatican makao makuu ya ukatoliki, mahali ambapo ajenda za uongo huanzia. Covid19 ni janga lililopangwa tangu mda. Lakini kiongozi wa Vatican anatuambia kuwa, kwasababu ya kutoitunza jumapili ndiyo sababu MUNGU katuadhibu kwa covid19. Hakika #MUNGU Baba Yetu Muumbaji hausiki na covid19, anazushiwa tu na kiongozi wa Vatican .
Sasa naiuliza Vatican hivi👇🏻👇🏻
Je ni kweli Mungu mnayemsema alituagiza kuitunza #Jumapili??
Bwana Mungu hebu atupatie majibu kutoka katika biblia neno lake.
Kutoka 20:8-11👉🏻ikumbuke siku ya sabato.
Kumbukumbu la Torati 5:12-15👉🏻ikumbuke siku ya sabato.
Isaya 66:22-23👉🏻sabato hata sabato wanadamu wote watakusanyika kuabudu katika mbingu mpya na nchi mpya.
Isaya 58:13-14👉🏻usigeuze mguu wako kuihalifu sabato
Ezekiel 20:12-13👉🏻sabato ni ishara kati ya MUNGU na watu wake.
Luka 4:16👉🏻 Yesu aliitunza sabato
Marko 6:1-2👉🏻Yesu yuko ndani ya sinagogi akihubiri siku ya sabato
Marko 16:1,9 👉🏻Sabato ilipoisha, wanajiandaa kwenda kwenye kaburi la Yesu. Alfajiri jumapili siku ya kwanza ya juma Yesu anafufuka.
Matendo 17:1-2👉🏻paulo mtume aliitunza sabato. Matendo 16:13 wakristo wa kwanza waliitunza sabato.
Matendo 13:44👉🏻watu wengi walikusanyika na paulo kuabudu.
Sasa Vatican ituambie ni wapi MUNGU kasema tuitunze #jumapili???🤔🤔
Naamini Viongozi wa Vatican hawana majibu isipokuwa majibu ya kulazimisha tu watakuwa nayo.
Katika BIBLIA yote hakuna mstari hata mmoja ambao MUNGU kaamuru Wanadamu kuitunza jumapili ili waepukane na covid19 na mabadiliko ya tabia ya nchi(climate change ) Hakuna.
Manabii, wafalme, mitume ,Yesu na woote waliitunza sabato.
Kuna wakati tunapaswa kumpinga shetani kwa neno la MUNGU bila kuogopa. Shetani anawatumia wanadamu waovu kufikisha ajenda zake, MUNGU pia anatumia Wanadamu watiifu kufikisha ajenda zake, hivyo Pambano Kuu ni kati ya KRISTO na watu wake dhidi ya shetani na watu wake.
Kumbe lockdown zote tunazozisikia duniani ni mpango wa Vatican . Covid19 siyo pigo kutoka kwa MUNGU ila ni mpango ulioandaliwa kwa siri ili kuwatisha wanadamu na kuwalaghai ili wamsujudie shetani. Kuusujudia upapa ni kumpa shetani heshima. Hizi ajenda za covid19 na mabadiliko ya tabia nchi ni ajenda kutoka Roma. Ajenda za kuleta sabato bandia ili kuwakosesha wanadamu ili washindwe kutambuwa unabii unavyotimia. Ukifikiria kwa haraka hizi ajenda utaona kuwa ni jambo zuri kabisa la kuiokoa sayari dunia, lakini ni ajenda chonganishi kati ya MUNGU na wanadamu.
Wapendwa, mambo ni mengi, tuweni macho. Mengine yanaingizwa makanisani mwetu na kupigiwa debe na viongozi, angalieni sana, someni dalili za nyakati. Hali ya mambo duniani siyo salama, hasa kwa wacha MUNGU wa kweli.
Chunga sana. Saa mbaya Yaja.
Mtafuteni BWANA kwa bidii.
Mubarikiwe.
Post a Comment