KIKAO CHA PAWEL JABLONSKI NA VIONGOZI NCHINI
Mhe. Pawel Jablonski, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland anayeshughulikia Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo kwa nchi za Afrika na Mashariki ya Kati amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.), Waziri wa Fedha na Mipango; Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), Waziri wa Viwanda na Biashara; Mhe. Exhaud Kigahe (Mb.), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara; na Mhe. Hussein Bashe (Mb.), Naibu Waziri wa Kilimo.
Madhumuni ya kufanya kikao hicho ni kujadili uwekezaji unaofadhiliwa na Serikali ya Poland nchini hususan changamoto zinazokabili uwekezaji kwenye miradi inayohusu kiwanda cha kuunganisha Matrekta (unaotekelezwa na kampuni ya Ursus ya Poland); na ujenzi wa maghala (unaotekelezwa kwa pamoja kati ya kampuni ya Unia na Feerum za Poland).
Kikao hicho changamoto mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na; baadhi ya makampuni ya Poland (Ursus na Feerum) kutotimiza matakwa ya mkataba iliosainiwa kati yao na Serikali ya Tanzania;
Katika kutatua changamoto hizo, viongozi hao wa pande zote mbili wameonesha nia ya dhati ya kutatua changamoto hizo.
Aidha, Viongozi hawa wamekubaliana kuundwa kwa kikosi kazi kujadili changamoto hizo kitaalam na kushauri namna ya kuzishughulikia.
Kikosi kazi hicho kihusishe wataalam kutoka upande wa Tanzania na Poland. Kadhalika, kikosi kazi hicho kimetakiwa kuanza kazi mapema iwezekanavyo.

Post a Comment