Advertisement

Responsive Advertisement

KAYA NA FAMILIA LEO 16

*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*

*KAYA NA FAMILIA.*

TRH. 16/06/2021.

DEVOTHA SHIMBE.

*SOMO: VIKWAZO VINAVYOWEZA KUONDOA SHANGWE KATIKA NDOA.*

Leo tutaangalia vikwazo katika ndoa pamoja na suluhisho la vikwazo hivyo. Tangu mwanzo Mungu alikusudia wanandoa wawe na furaha na shangwe. Lakini kwa sababu ya Ibilisi mfumo wote ukabadilika bado lipo tumaini hata sasa.

Mahusiano huleta furaha, amani hasa pindi unapokuwa na mwenzako.

Miongoni mwa vikwazo hivyo ni pamoja na hivi

Mawasiliano, pesa, matarajio, mahusiano kingono, utofauti wa haiba, kazi nyingi na ratiba ngumu, malezi ya watoto, umri wa ndoa, kuishi na ndugu.

1. Mawasiliano.

Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; 
Yakobo 1:19

kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. 
Yakobo 1:20

2. Suala la pesa. 
Hii nayo ni changamoto kwa hakika. Madeni na mikopo ni shida kubwa. Au mwingine ana kipato kikubwa mwingine kidogo. Je ni nguvu ya pesa au ni nguvu ya upendo ndiyo inaongoza familia? Mbinu za uwekezaji ni za namna gani.

3. Ndugu zako.
Kuishi na ndugu yaweza kuwa ni tatizo.

4. Matarajio. Je, ulivyooa na sasa hali ikoje? Je ulitarajia nini? Au yuko sawa.

5. Mahusiano kingono. Mpango wa Mungu ni mume na mke pekee na siyo vinginevyo. Suala zima la kuridhishana katika ndoa haliko vizuri. Wengi hufika safari zisizo za kwao hivyo huishia njiani, sasa katika hali kama hii ndoa haiwezi kuwa na furaha. Na hii hupelekea kuchokana, wengine kutothaminiana.

6. Tofauti za haiba. Wengine ni waongeaji, wengine ni wakimya. Sasa hii inaweza kuleta shida katika ndoa. Wengine wacheshi. 

7. Kazi nyingi. Hizi hukosesha muunganiko wa kuwa pamoja. Mwingine yuko Mwanza, mwingine Dodoma. Kipi bora kati ya ndoa na kazi? Jiulize swali hili. Mgawanyo wa majukumu kutokwenda sawa ni tatizo pia mwa wanandoa.

8. Malezi ya watoto. Watoto wanahitaji malezi ya wazazi wote nyumbani.

9. Ndugu katika familia(Extended family) wakwe, mashemeji nk.

Ili dini iwepo katika jamii ni lazima ilete mvuto katika nyumba yako kwanza.(EGW. ADVENTIST HOME)

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.

Post a Comment

0 Comments