Advertisement

Responsive Advertisement

HIJJA 2021 YAFUTWA

MUFTI na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar bin Zubeir, amesema Saudi Arabia imefuta ibada ya hijja kwa mwaka huu kufuatia uwepo wa janga la covid-19 kwenye nchi nyingi duniani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam JANA, Juni 16, Sheikh Abubakar amesema taarifa hiyo rasmi imetolewa na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Abdul Aziz Hamad.

"Kutokana na taarifa niliyopata hakutakuwa na hija mwaka huu, isipokuwa itatekelezwa na wenyeji Saudi Arabia ambao ni wakazi wa palepale kutokana na maambukizi ya virusi vya corona," amesema Mufti.

Hii ni mara ya pili kwa waumini wa dini ya Kiislamu nje ya Saudia, kutotekeleza nguzo hiyo ya ibada, baada ya mwaka jana pia kuahirishwa, kutokana na ugonjwa huo ulioanza Desemba 2019, nchini China na kuenea maeneo mengine ya dunia.

Post a Comment

0 Comments