Advertisement

Responsive Advertisement

GHARAMA ZA BLOG, YOUTUBE KUSHUKA

Serikali imesema itabadilisha kanuni ya tozo za usajili wa leseni za maudhui mtandaoni ili kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kutumia vipaji vyao kwa maslahi ya taifa.

Imesema serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia, inataka taasizi zake ziwe walezi wa sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano siyo kama polisi wa sekta.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma Jana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile, akizungumza kwenye mkutano kati ya wizara hiyo, taasisi zake na wahariri wa habari.

Ndugulile alisema serikali imewekeza kiasi cha sh. bilioni 677, katika ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTTB) na kwamba kuna umuhimu wa mkongo huo uwe na manufaa kwa jamii hususan vijana.

"Tumekuwa na vijana wabunifu lakini tunaua vipaji vyao kwa kuweka tozo kubwa. Leo unamwambia kijana atoe sh. milioni moja, ataipata wapi," amehoji Waziri Ndugulile.

Kwa mujibu wa Kanuni za Matumizi ya Mtandao, usajili wa maudhui mtandaoni yanaanzia sh. 100,000 hadi sh. milioni moja, huku kutangaza mubashara mtandaoni kwa redio na runinga, gharama zikiwa kati ya sh. 50,000 hadi sh. 200,000.


Post a Comment

0 Comments