Advertisement

Responsive Advertisement

DIWANI ARIDHISHWA UJENZI WA BARABARA DSM

Diwani Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule, amesema ameridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi wa barabara unaoendelea eneo la Akha Khan, Dar es Salaam.

Ametoa kauli hiyo, alipotembelea eneo hilo leo, Juni 16, 2021, kwa lengo la kukagua ujenzi wa barabara hiyo, ambayo iko ndani ya kata yake.

Diwani huyo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri anazozifanya, kuhakikisha maendeleo endelevu kwa Watanzania.

Ameupongeza Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), kwa usimamizi makini wa ujenzi wa Daraja la New Selander, ambao uko katika hatua za mwisho.

Post a Comment

0 Comments