HALMASHAURI YA ARUSHA KUSIMAMIA MAZINGIRA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Arusha kusimamia vizuri usafi wa mazingira kwa kudhibiti utupaji wa taka kando ya Mto Themi unaotiririsha maji yake kijiji cha Bwawani wilayani Arusha.

Ametoa maelekezo hayo kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Bwawani wilayani Arusha ambapo taka hizo husombwa na maji hadi kijijini hapo na kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho pamoja na mambo mengine, amesema kuwa Jiji la Arusha linapaswa kuwa katika hali ya usafi zaidi ili kuwa jiji la mfano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Naibu Waziri ameelekeza wananchi kuacha kufanya shughuli za kiuchumi kando ya mto Themi hali inayochangia uharibifu wa kingo za mto na Themi hali inayochangia uharibifu wa kingo za mto na mmomonyoko wa udongo.

No comments