Shirikisho la Soka Nchini Uganda, FUFA imetangaza kuwa mechi zote za Ligi Kuu ya Uganda zilizopangwa kufanyika wikendi hii zimeahirishwa.
Katika harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini Uganda, Rais Museveni alirekebisha maagizo yake aliyotoa Ijumaa na kuongeza vizuizi nchini.
"FUFA inapenda kutangaza kwamba mechi zote za Star Times UPL zilizopangwa kufanyika Jumamosi tarehe 19 Juni 2021 na Jumapili tarehe 20 Juni 2021 zimeahirishwa"
"FUFA itatoa mwongozo zaidi juu ya siku zilizosalia za mechi siku za usoni. Ni Mchezo Wetu, Ni Nchi Yetu , "taarifa kutoka FUFA ilisomeka kupitia akaunti yao rasmi ya Twitter.
#
0 Comments