WAUZA MATUNDA WAONDOLEWA SOKONI NCHINI UGANDA
Moja ya PICHA iliyonaswa na watu Nchini Uganda leo Juni 19, 2021 inaonyesha maafisa wa polisi wakiwaamuru wachuuzi wa matunda waondoke katika mitaa ya jiji la Kampala baada ya Rais Museveni hapo jana Juni 18 kutangaza hatua mpya za kudhibiti kesi zinazoibuka za #COVID19.
Vifo vya Raia 234 ndani ya mwezi mmoja kutokana na mlipuko wa #COVID19 vimepekea Rais Yoweri Museveni kutangaza masharti mapya
Wananchi watatakiwa kuwepo ndani kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja na nusu alfajiri
Safari za Umma na Binafsi kati ya Wilaya zimepigwa marufuku kwa siku 42.
Rais Museveni amesema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa #Entebbe utakuwa wazi lakini hawatoruhusu Virusi kuingia Uganda.
Maeneo yote ya Ibada, Shule na Taasisi za Elimu zitafungwa kwa siku 42 huku matukio ya Michezo nayo yakisitishwa.
Post a Comment