CHAMA; TUNAMSHUKURU MUNGU
Wiki chache zilizopita zimekuwa ngumu sana kwangu na familia yangu baada ya kuondokewa na mpendwa wetu- Mercy, lakini yote kwa yote tunamshukuru Mungu mwenye sababu ya kila kitu kinachotokea maishani mwetu.
Siku hizi za majonzi zingekuwa ngumu zaidi kama isingekuwabmsaada wenu wa dhati ambao mmekuwa mkinipatia.
Mmelia na mimi na zaidi ya yote mmeniombea, na nathubutu kusema kuwa maombi yenu yametufariji mimi na familia yangu kwa kiasi kikubwa.
Nipende kuushukuru uongozi wa klabu ya Simba SC chini ya Mo Dewji na Barbara Gonzalez kwa kunishika mkono katika kipindi ambacho nilikuwa nikiwahitaji zaidi.
Shukrani za dhati ziwaendee wachezaji wenzangu na mashabiki wa mpira ulimwenguni kote kwa kuwa na mimi bega kwa bega.
Ni katika kipindi kama cha maisha yako unaweza kujua ukubwa na ubora wa familia iliyokuwa nyuma yako.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipoushukuru uongozi wa Lusaka Dynamos, klabu yangu ya zamani, pamoja na Wana Zambia wote ambao waliungana na mimi kumpumzisha mke wangu mpenzi kwenye nyumba yake ya milele.
Ni vigumu kumtaja kila mmoja aliyeshiriki katika kunifariji lakini Mungu wangu wa mbinguni atawabariki wote kwa kuwa anajua jinsi mlivyoniunga mkono kuliko hata nijuavyo mimi.
Amani ya milele imuangazie mke wangu mpendwa. Hayupo kimwili lakini tupo naye kiroho na anaishi miongoni mwetu kila siku.
Amina!
----->@realclatouschama Clatous Chota Chama, Kiungo wa Klabu ya Simba SC na Timu ya Taifa ya Zambia.
Post a Comment