BITEKO AZINDUA JUKWAA LA WADAU WA MADINI KUPITIA NMB
Waziri wa Madini Doto Biteko amezindua rasmi Jukwaa la Wadau wa Madini kupitia Benki ya NMB lenye lengo la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara, wachimbaji na wadau wa madini ili kuwa na sauti moja katika kujadili changamoto wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.
Hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa hilo unaokwenda kwa jina la NMB MINING CLUB umezinduliwa tarehe 28 Juni, 2021 katika Hotel ya Morena Jijini Dodoma na kuhuhudhriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Biteko amesema kuwa, ili kuwarahisishia wachimbaji kupata mikopo kwa urahisi katika mabenki ikiwemo vifaa vya uchimbaji, Wataalam wa Wizara ya Madini hawanabudi kutoa ushirikiano kwa mabenki pindi yanapohitaji msaada wa kitaalamu ili yaweze kutoa mkopo kwa wateja wao kwani baadhi ya mabenki yameshindwa kutoa mkopo kwa wachimbaji kutokana na kukosa elimu ya kutosha kuhusu sekta ya madini.
" Ninatoa rai kwa mabenki nchini kuungana kwa pamoja na kutoa mikopo mikubwa kwa wawekezaji wakubwa wa madini wanaotaka kuwekeza nchini ili faida inayotokana na mikopo hiyo ibaki nchini," amesema Waziri Biteko.

Post a Comment