AMKA NA BWANA LEO 7

KESHA LA ASUBUHI

Jumatatu 07/06/2021

*NEEMA YAKE YATOSHA*

*Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.* Wafilipi 2:12,13

☄️ Kila mmoja wetu ana kazi ya kufanya katika wokovu wetu, ambayo ni kukidhi kila matakwa ya Mungu. Mungu hafanyi kitu chochote bila kutumia wakala ambaye kazi inafanywa kwa ajili yake. Neema Yake yatosha kufanya kazi ndani yao na pamoja na wale ambao ni wa Kwake, katika utimizaji wa kila ahadi, wakati yule ambaye neema hii imetolewa kwake anapaswa kutii kila amri. 

☄️ Matokeo ya madai ya Mungu ni kuwasababisha watu wake watoke duniani na wajitenge, wasiwe na ushirika na kazi za giza zisizokuwa na matunda. Bila utakatifu “hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14). “Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.” (Yakobo 4:4). 

☄️ Wakati Bwana anafanya kazi pamoja nasi tunapaswa kufanya kazi kwa ajili yetu. Wakati Bwana anawatuma watumishi Wake kwa makemeo, kwa tahadhari, kwa maonyo, hatupaswi kugeuka nyuma na kukataa kupokea ujumbe kwa sababu hautoki kwa watu wenye elimu. Hatupaswi kusema, ujumbe huu hauhitajiki. Kila ujumbe unaotumwa kwako na mjumbe wa Mungu kwa ajili ya mema yako, ili kukufundisha njia ya wokovu kwa ukamilifu zaidi. Ni njia gani ambayo Mungu ataitumia kuwasiliana na wanadamu, isipokuwa kupitia wajumbe wake? Je, huogopi kuchagua sehemu hiyo ya ujumbe ambayo inakupendeza na kukataa ule ambao unafunga njia zako? 

☄️ Hupaswi kuonesha mashaka yako. Huo ni udanganyifu wa Shetani. Ikiwa hutumii njia na nyenzo ambazo Mungu ametumia ili kukufikia, je, utafikiria ana njia gani iliyosalia ili kushughulikia suala lako? Je, hakukuwa na kosa kabisa kuwakosoa watumishi wa Mungu, kuongea kwa urahisi kuhusu wale ambao mtume amewaunganisha kwako ili uwajali sana kwa ajili ya kazi yao? Je, wanaume na wanawake wenye uzoefu mdogo sana watakataa kusaidiwa na nyenzo ile ile ambayo Mungu ameiweka, watumishi Wake?.

🔘 *Ni heshima ya namna gani ambayo unadhani watoto wako watakuwa nayo kwa wajumbe wa Mungu baada ya kuwasema bila heshima watu hawa kama ulivyofanya?*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments