AMKA NA BWANA LEO 29

KESHA LA ASUBUHI

JUMANNE, JUNI, 29, 2021
SOMO: TWENDE KWA NANI? 

Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. 

Matendo 4:11, 12. 



Wakati wafuasi wengi wa Kristo walipomwacha, na Mwokozi akawauliza thenashara, “Ninyi nanyi mwataka kuondoka?” Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele” (Yohana 6:68). Yesu alijawa huzuni kuona mtu yeyote anamwacha, kwa sababu alijua kwamba imani kwa jina Lake na utume Wake ni tumaini pekee la mwanadamu. Hatua hii ya wafuasi wake kumwacha lilikuwa ni suala la kumuumiza. Ni kidogo kwa jinsi gani binadamu wanajua huzuni iliyojaza moyo wa upendo usio na kikomo wakati mambo hayo yalipotokea. 



Hakuna mtu duniani ambaye alitamani kwa dhati kuthamini na ushirika kuliko ambavyo Kristo alitamani. Alitamani huruma. Moyo wake ulijazwa na shauku kubwa kwamba mwanadamu athamini karama ya Mungu kwa ulimwengu, na kumheshimu kwa kuyaamini maneno yake na kuzungumza sifa yake. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16). 



Maneno, “Ninyi nanyi mwataka kuondoka?” yalikuwa yanaonesha majuto kiasi gani. Yaligusa mioyo ya wanafunzi wote isipokuwa mmoja. Na mmoja huyo alikuwa Yuda. Moyo wake ulikuwa ni kwa ajili ya pesa tu. Shauku yake kubwa ilikuwa kuwa mtu mkubwa sana. 



Wanafunzi walisema, “Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.” Angalia vile Kristo alivyokuwa. Mwana wa Aliyejuu kabisa, lakini akawa mtu wa huzuni aliyezoea sikitiko. Je, tumewahi kushuhudia baraka inayokuja kwa kumwamini kwa moyo wote, na kumtukuza kwa kuonesha upendo wetu na ibada kwake? Kristo ana njaa ya matunda, tunda ambalo litatuliza njaa yake ya roho kwa niaba yetu. Ni shauku yake kwamba tubebe "matunda mengi."



Hebu tufungue mioyo yetu kwa upendo Wake. “Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?” (Marko 8:36). Tutakapoweza kuzungumza tukiwa na ufahamu na maneno yaliyosemwa na Petro, “Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele,” baraka za ajabu zitatufuata.



—Barua ya 171, Juni 29, 1905,, kwa Edson na Emma White.

No comments