AMKA NA BWANA LEO 28

KESHA LA ASUBUHI

JUMATATU, JUNI, 28, 2021
SOMO: TAA YA NJIA YETU 

Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga ..... Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki. 

Zaburi 119:130—133. 



Nilimwona malaika wa Mungu amesimama pembeni yako, akikuelekeza juu. Malaika huyu alimhudumia baba na mama yako, na amekupatia ulinzi wake lakini mara nyingi umekuwa ukimwepuka, na umekuwa ukitafuta kufuata njia zako mwenyewe. Kwa hiyo umetanga mbali na Mungu. 



Heri mtu yule ambaye amegundua kuwa Neno la Mungu ni nuru katika miguu yake na taa ya njia yake—nuru inayong’aa gizani. Ni ramani ya mbinguni kwa wanadamu. Lakini kuna watu wengi ambao hawana kiongozi zaidi ya maoni ya wanadamu wenye ukomo, kiburi, tamaa au hisia zao wenyewe zinazobadilika. Akili zao zipo katika hali ya kusumbuliwa na kutokuwa na uhakika. Daima wanateseka kwa homa ya akili. 



Kama ungekuwa unamfuata Kristo, Neno la Mungu lingekuwa kwako kama nguzo ya wingu wakati wa mchana na nguzo ya moto wakati wa usiku. Lakini hujafanya kumheshimu Mungu kuwa kusudi la maisha yako. Una Biblia. Isome na ujifunze. Mafundisho ya mwongozo wa kiungu hayapaswi kupuuzwa au kupotoshwa. Ufahamu wa kiungu utawaongoza wale ambao wanatamani kuongozwa. Ukweli ni ukweli, utawafumbua wale wote ambao wanautafuta kwa moyo mnyenyekevu. Kosa ni Kosa, na hakuna falsafa yoyote ya kidunia ambayo inaweza kufanya liwe kweli.



“Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:20). Mungu anataka nini kwa urithi wake alioununua kwa damu? Utakaso wa mtu mzima—usafi kama usafi wa Kristo, kufuata mapenzi ya Mungu kikamilifu. Ni kitu gani hicho ambacho kinajumuisha uzuri wa roho? Uwepo wa Neema yake Yeye ambaye aliyatoa maisha Yake ili awakomboe wanadamu dhidi ya mauti. 



Hakuna hali ya kusihi iliyo ya upole, hakuna masomo ambayo ni dhahiri sana, hakuna amri yenye nguvu sana na inayolinda, hakuna ahadi ambayo ni kamilifu, zaidi ya zile ambazo zinamwelekeza mwenye dhambi katika chemchemi ambayo imefunguliwa ili kufutilia mbali hatia ya roho ya mwanadamu.



—Barua ya 207, Juni 28, 1904,, kwa jamaa wa siku za Battle Creek.

No comments