AMKA NA BWANA LEO 27
KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI, JUNI, 27, 2021
SOMO: NGUVU YA MAOMBI
Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
2 Petro 3: 9.
Ni jambo la kushangaza kwangu kwamba Mungu atauvumilia uovu wa wanadamu kwa muda mrefu, anastahimili kutotii kwao lakini bado anawaacha waendelee kuishi, wakitumia vibaya rehema zake, wakimshuhudia uongo katika kauli za uovu sana. Lakini njia za Mungu si njia zetu, na hatutashangaa ustahimilivu wake wa upendo na huruma na kujali kusikokoma, kwa maana ametoa ushahidi usiopingwa kwamba hii ndiyo tabia Yake —si mwepesi wa hasira, akionesha rehema kwa maelfu ya wale wampendao na kutunza amri zake.
Ninashukuru sana kwa utulivu mzuri ninaoufurahia asubuhi hii. Nilipumzika vizuri usiku uliopita na ninahisi kuipumzisha roho yangu kwa Mungu asubuhi hii. Hataniacha wala kunikataa. Kwangu atakuwa msaada uliopo wakati wa shida....
Roho zinapotea katika dhambi zao kila upande. Moyo wangu unawaonea shauku sana. Ninatamani niwaamshe watoke katika usingizi wao wa mauti. Ni wangapi ambao bado hawajaonywa, ambao hawajawahi kuusikia ukweli; wakati maonyo na maombi yanasikika katika masikio ya wengine ambao hawazingatii, bali wanakataa upendeleo na fursa ambazo zingekuwa kwa ajili ya wokovu wao ikiwa watafaidika nazo. Wanaonekana wamefungwa na barafu. Lakini mioyo yetu inapaswa kuonywa kwa moto wa kiungu; jitihada zetu za Kikristo na mfano wetu wa Kikristo unapaswa kuwa wa dhati na wenye nguvu.
Majukumu tuliyonayo si madogo. Hali yetu ya kuwa tegemezi itatusogeza karibu na Mungu, na ufahamu wetu wa majukumu ya kutekelezwa utatufanya tuwe na jitihada, zikiunganishwa na maombi yetu ya dhati, matendo, imani na maombi daima. Nguvu! Nguvu! Kilio chetu kikubwa ni nguvu bila kipimo! Inatusubiri. Tunapaswa tu kuchukua, kuliamini neno la Mungu, kutenda imani; kusimama imara, kuzishikilia imara ahadi; kupigana ili tupewe neema ya Mungu. Elimu si muhimu, akili nyingi si lazima; unaweza usiwe mzungumzaji mzuri; lakini maombi ya moyo mnyenyekevu uliopondeka Mungu anayasikia, na anapoyasikia hakuna kikwazo duniani kinachoweza kuzuia. Nguvu ya Mungu itatufanya tuwe na ufanisi.
—Barua ya 35, June 27,1878,, kwa mwenyekiti wa Makao Makuu ya Kanisa Ulimwenguni, mume wake.
Post a Comment