AMKA NA BWANA LEO 23
KESHA LA ASUBUHI
Jumatano 23/06/2021
*NAMNA MUNGU ANAVYOSHUGHULIKA NA WATU*
*Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?* *Yakobo 2: 5*
Katika mfano wa mtu tajiri na Lazaro, Mwalimu mkuu anafungua pazia, akionesha kwamba Mungu ni msingi wa imani yote, wema wote, rehema yote.
Wayahudi walidai kuwa ni wazao wa Ibrahamu, lakini walishindwa kufanya matendo ya Ibrahimu, walithibitisha kwamba hawakuwa watoto wake wa kweli. Ni wale tu ambao wanaunganika naye kiroho ndio wanaohesabiwa kuwa wazao wake wa kweli. Kristo alimtambua ombaomba [Lazaro] kama ambaye Ibrahimu atamthamini sana kama rafiki, ingawa alikuwa katika tabaka ambalo linadharauliwa na wanadamu.
*Huruma ya kibinadamu yapasa kuwa katika kila moyo*. Ni tabia ya Mungu na haipasi kufukuzwa. *“Nanyi nyote ni ndugu” (Mathayo 23:8). Mungu amewapatia wanadamu jukumu la kuonesha huruma kwa wanadamu wenzao, kuwasaidia wahitaji,waliojeruhiwa, walioumizwa*. Wengi wameharibiwa kwa matendo yao wenyewe, lakini ni nani katika jamii ya wanadamu anaweza kuelewa, kama ambavyo Mungu anaelewa, sababu ya mateso yao?
Katika ulimwengu wetu leo kuna watu wengi ambao wamejeruhiwa, mioyo isiyo na furaha inayohitaji unafuu. Bwana ana mawakala wa kuyaangazia maisha hawa waliokata tamaa. Kila mmoja wetu anaweza kutumia karama zake kwa kuzalisha riba kwa kuyaondoa mawingu na kuiruhusu nuru ya matumaini na imani kwa Yule ambaye *“aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16)*.
*Kristo ametuonesha kwamba kuna wakati unakuja wakati nafasi za matajiri ambao hawakumfanya Mungu kuwa tegemeo lao, na masikini ambao wamemfanya Mungu kuwa tegemeo lao, watabadilishana nafasi. Wale ambao ni masikini wa vitu vya dunia hii, lakini wale ambao ni wastahimilivu katika mateso, na ambao wanamwamini Mungu, siku moja watainuliwa juu ya wengi ambao wanashikilia nafasi za juu kabisa ambazo dunia hii inaweza kuzitoa.
*Bwana hashughuliki nasi kama wanadamu wanavyofanya.Alimtoa Mwana wake kwa kafara kubwa sana, ili aweze kutuvuta katika huduma Yake, na kupitia kwake alitoa mbingu yote. Alifanya hivi ili kuonesha thamani aliyoiweka kwa viumbe aliowaumba.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*
Post a Comment