AMKA NA BWANA LEO 21
KESHA LA ASUBUHI
Jumatatu 21/06/2021
*MWALIKO KWA WOTE*
*Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.* Luka 10: 2
Nimekuwa siwezi kusafiri kwa kipindi fulani sasa, kwa sababu ya matatizo ya nyonga na uti wa mgongo, na wakati narejea nyumbani [kutoka katika Chuo cha Healsburg] nilichoka kweli. *Lakini ninamshukuru Baba yangu wa mbinguni Yeye anayenipa nguvu.*
Hivi karibuni mikutano ya hadhara imefanywa na ndugu zetu huko Calistoga [California]... Unaofuata utafanyika karibu na St. Helena, ikiwa eneo zuri litapatikana.Tunatamani kufanya yote tunayoweza ili kuwaonya wale wanaotuzunguka juu ya kukaribia kuja kwa Mwokozi. Ninaamini mazuri mengi yatakamilishwa tutakapoifanya hii kazi. Moyo wangu unavutwa kwa wale ambao wapo gizani, ambao hawaujui ukweli.
Ninatarajia hivi karibuni kutembelea makazi ya wanajeshi huko Yountville. Kwa miezi kadhaa kundi la wafanyakazi limekuwa likienda kila baada ya Sabato moja ili kutoa huduma ya kuimba. Mwanzoni ni watu wachache tu ndio walihudhuria huduma hiyo, lakini sasa wanaanzia watu sabini na watano hadi mia moja wanaokuja kila wakati. Wakati mwingine mazungumzo ya dakika 30 kuhusu mada za Biblia hutolewa.
Katika mkutano uliofanywa wiki chache zilizopita, wanajeshi waliulizwa ikiwa wangependa kuwa na masomo mafupi ya kujifunza Biblia baada ya huduma ya nyimbo. Zaidi ya watu kumi walikubali. Lakini wakati ulipofika wa kusoma, zaidi ya watu hamsini walikuwepo. Wafanyakazi wanakwenda na masomo ya kujifunza, na wanajeshi wanapoulizwa ikiwa watapenda kuyapata, nyuso zao zinachangamka na wananyoosha mikono yao kwa shauku ili kupokea vitabu na vijizuu.
Sabato iliyopita mtu mmoja aliyeonekana msomi katika makazi hayo alimwambia mmoja wa ndugu zetu, “Kabla hamjaja hapa kutuimbia, nilitumia karibu muda wangu wote kunywa pombe na kushereheka pamoja na wenzangu. Lakini tangu muanze kuja hapa, nimepata njia bora zaidi ya kutumia muda wangu. Nimeacha kunywa pombe na ninatumia muda wangu wa ziada kusoma kitabu cha Tumaini la Vizazi Vyote.
*Tunatumaini kwamba kazi kwa ajili ya wanajeshi itasonga mbele. Watu kadhaa wamevutiwa, na wale wanaosimamia makazi haya wanatambua kazi njema inayofanywa. Ninaamini kabisa kwamba baadhi ya watu wazima hawa, pengine wangi, wataokolewa.Ninatamani kuona watu wetu wote waone milango mingi iliyofunguliwa mbele yao.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*
Post a Comment