Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 17

KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, JUNI, 17, 2021
SOMO: HEBU TUSHIKILIE SANA TULICHO NACHO 

Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 

2 Wakorintho 12: 9. 



Usiku uliopita nililala kidogo sana. Nilijaribu kumtazama Yesu nijiweke katika mikono ya Tabibu Mkuu. Amesema, “Neema yangu inakutosha” (2 Wakorintho 12:9). Neema ya Kristo inawafanya wanadamu wazungumze maneno sahihi katika hali zote. Mateso ya kimwili si kisingizio cha kufanya matendo yasiyo ya Kikristo. 



Katika saa hizi ambazo sikupata usingizi, suala la ushindi lilikuwa mzigo wa mawazo yangu. Bwana alitangaza, “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi” (Ufunuo 3:21). 



Kuna wale ambao daima wanatoa visingizio kwa kufuata mashauri ya adui. Wengine wanadhani kwamba kwa sababu wana udhaifu wa kimwili, wana pendelewa kuzungumza maneno yasiyo na maana na kutenda kwa namna isiyo nzuri. Je, Yesu hakuweka njia kwa ajili ya watu hao washinde majaribu? Kwa sababu ya majaribu na mateso, je, wanapaswa kutokuwa na shukrani na kutokuwa watakatifu? Je, miale ya haki ya Kristo si angavu kuweza kuondoa kivuli cha shetani?



Neema ya Mungu imetangazwa kuwa inatosha kwa magonjwa na majaribu dhidi ya yale ambayo wanadamu wanapambana nayo. Je, haina nguvu dhidi ya udhaifu wa mwili? Je, neema ya Mungu irudi nyuma, huku Shetani akichukua uwanja, akimshikilia mateka kwa uwezo wa tabia yake ya uovu? 



Yesu ni wa thamani kiasi gani kwa mtu ambaye anamtumaini! Lakini wengi wanatembea katika giza kwa sababu wanazika imani yao katika kivuli cha Shetani. Hawajafanya kila ambacho kilikuwa ndani ya uwezo wao kufanya kupitia neema ya Yesu. Hawajazungumza kuhusu imani na matumaini na ujasiri. Hatupaswi kumruhusu Shetani hata kwa wakati mmoja afikiri kwamba uwezo wake wa kufadhaisha na kusumbua ni mkubwa kuliko uwezo wa Kristo kushikilia na kuimarisha. 



“Watu imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.” (Luka 18:1). Kila ombi la dhati linalotolewa kwa Mungu linachanganywa na ufanisi wa damu ya Kristo. Ikiwa jibu limechelewa, ni kwa sababu Mungu anatamani tuoneshe uimara mtakatifu katika kudai ahadi ya Mungu. Yeye aliyeahidi ni mwaminifu.



—Manuscript 19, Juni 17, 1892 ....

Post a Comment

0 Comments