TAGCO WAMPA TUZO DKT. HASSAN ABBAS
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ametunukiwa tuzo na Chama cha Maafisa
Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa
kutambua mchango na mageuzi makubwa aliy-
oyafanya kwenye Sekta ya Habari hapa nchini.
Akikabidhi tuzo hiyo kwa Dkt. Hassan Abbasi,
Mwenyekiti wa TAGCO, Paschal Shelutete wakati
wa kikao cha 16 cha TAGCO kilichofanyika Jijini
Mbeya Mei 24,2021 amesema Dkt. Abbasi
ametoa mchango mkubwa akiwa Mkurugenzi wa
Idara ya Habari- MAELEZO na Mkuu wa Serikali
tofauti na hapo awali.
"Ni katika kipindi hiki ambapo miradi ya kimkaka-
ti ya Serikali ilisemewa vizuri zaidi na kufahamika
na watu wengi hivyo kuwafanya wananchi kuipen-
da Serikali yao" Amefafanua Shelutete.
Waandishi kwa kumpa tuzo hiyo na kuahidi
kuendelea kuwapa ushirikiano ili waweze
kuendelea kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo
"Tuendelee kushirikiana katika cheo hiki kipya
cha Katibu Mkuu katika Wizara yetu ambayo
ni Wizara muhimu inayogusa umma kwa nyanja ya burudani na huzuni kutokana na Sekta zake" Ameongeza Dkt. Abbasi.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini na kumrejesha tena kwenye nafasi ya Katibu Mkuu
na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na bidi ili
kutekelea Ilani ya Chama cha Mapinduzi na maelekezo ya Mhe. Rais Samia.
Post a Comment