WIZARA ZATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU
imetekeleza maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimi-
wa Kassim Majaliwa Majaliwa Mei 21, 2021 wakati akizindua Kongamano la kuenzi mchango wa Tanzania kwenye Ukombozi wa Afrika Jijini Dar es Salaam ya kuitaka Wizara hiyo, Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutatua changamoto za kimuundo kwenye Sekta za Utamaduni na Michezo.
Katibu Mkuu wa Habari Dkt. Hassan Abbasi ameongoza kikao hicho kilichoshirikisha MakatibunWakuu wa Wizara za TAMISEMI na Utumishi,bkwenye kikao kazi cha Maafisa Utamaduni nabMichezo nchi Tanzania Bara ambapo amesema maelekezo yote yamefanyiwa kazi na kukamilikabkilichobaki ni kuandaa nyaraka ili kufanikisha utekelezaji wa maelekezo hayo.
"Kikao hichi kimejadili na kutekeleza maagizo ya
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyotoa Mei
21, ikiwemo kufanya marekebisho ya Muundo wa
kada za Maafica Utamaduni na Michezo na tayari
kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na
Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora tumeyafanyia kazi" amesema Dkt. Abbasi.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Dkt.nFrancis Michael amefafanua kuwa muundonulioboreshwa unamtambua mtaalam mwenyenfani nyingine ambazo siyo za michezo lakininana uzoefu kwenye michezo na amepatanmafunzo ya michezo anakuwa na nafasi ya kuwa kwenye kada Afisa Michezo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli amesema kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo kitaundwa na kitatengewa bajeti kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya sekta hizo ambapo amesisitiza maafisa haonkutekeleza majukumu yao kwa ufasaha ili waweze kupimwa utendaji wao kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Post a Comment