MAAFISA HABARI WATAKIWA KUZIJUA TAASISI ZAO

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt. Hassan amewataka Maafisa
Habari katika Wizara, Mikoa, Halmashauri,Taasisi,
Mamlaka na Wakala za Serikali kuzisemea taasisi
zao ili zitambulike kwa huduma wanazotoa kwa
wananchi.

Dkt. Abbasi amesema hayo alipokuwa akiwasili-
sha mada inayohusu "Mawasiliano ya kimkakati
ya Serikali katika Zama Mpya za Utekelezaji" Mei
27, 2021 Jijini Mbeya ambayo lengo lake ni kuwa
jengea uwezo maafisa hao waweze kusemea
taasisi zao kimkakati.

"Afisa Habari ni lazima uelewe taasisi yako, maelekezo mapya yanayoingia katika taasisi na
namna ya kuyafanyia kazi na mtambue jukumu
lenu ni kutoa taarifa kwa kuzingatia sheria za
ndani na nje ya nchi ikiwemo Mkakati wa Kimataifa wa Haki za kisiasa na kiraiam

Dkt. Abbasi ameongeza kuwa Serikali lazima
iaminike na kukubalika kwa wananchi wake,
hivyo utoaji wa taarifa utasaidia Serikali kuaminiwa na wananchi huku akisisitiza ukweli
katika kutoa taarifa kwa namna bora, kutumia
lugha sahihi na kutatua changamoto kabla
wengine hawajaziibua Lakini lazima Mamlaka
ya taasisi ishirikishwe".

Aidha, katibu Mkuu huyo ametoa msisitizo
kwa Maafisa Habari kwenda "field"kuona
taasisi inatekeleza nini kwa wananchi ili atoe
taarifa sahihi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hosptali ya Taifa Muhimbili Bw.
Aminiel Eligaesha alitoa pongezi kwa Katibu
Mkuu huyo kwa namna alivyofanya mageuzi
ya utoaji habari za Serikali kupitia vitengo vya
mawasiliano.


No comments