RAIS SAMIA AMEHUTUBIA BUNGE LA KENYA LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 05 Mei, 2021 amehutubia Bunge la Kenya lililojumuisha Bunge la Taifa na Bunge la Seneti ambapo ametoa wito kwa Wabunge hao kuchochea uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya.
Mhe. Rais Samia ambaye anakuwa Rais wa pili wa Tanzania kuhutubia Bunge la Kenya akitanguliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru Maspika na Wabunge wa Kenya kwa kukubali awahutubie na amebainisha kuwa huo ni uthibitisho wa udugu, urafiki, ujirani na nia njema ya Wabunge
na Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kukuza zaidi uhusiano uliopo na Tanzania Katika hotuba hiyo, Mhe. Rais Samia amesema haoni sababu ya Tanzania na Kenya kushindana bali anaona fursa ya kushirikimua zaidi katika uchumi kwa kuwa uhusiano wa nchi hizi ilioanza miaka 56 iliyopita sio wa hiari kutokana na kufungamanishwa uhusiano wa damu kwa jamii zilizopo pande zote, historia kutokana na kuwepo uhusiano hata kabla
ya uhuru nn jiografin kutokana na kuwa na mpaka mrefu na maeneo yenye rasilimali zilizoungana ikiwemno hifadhi na wanyama.
Ameahidi kuwa katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya unaimarika zaidi na ametoa wito kwa viongozi na watumishi wabSerikali kuendana na kasi ya ushirikiano waliyonayo wananchi kwani hivi sasa hali inaonesha wananchi wa Tanzania na wananchi wa Kenya wanashirikiana zaidi ikilinganishwa na namna viongozi na wafanyakazi wa Serikali wanavyoshirikiana.
Pia, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendeleza miradi ya ushirikiano ikiwemo
ujenzi wa barabara, ujenzi wa bomba la gesi la Dar es Salaam - Mombasa, ujenzi wa njia
ya umeme ya kilovati 400 kutoka Singida Tanzania kwenda Kenya, kukamilisha vituo vya
huduma za pamoja mpakani (One Stop Border Post na amesisitiza kuwa yeyote anayefikiria kuchonganisha Tanzania na Kenya ajue kuwa uhusiano wa nchi hizibulikuwepo, upo na utakuwepo sana.
Amewataka Wabunge hao kuwaongoza wananchi katika kuimarisha uhusiano huo badala ya kuadhohofisha na kwamba hata yeye amefanya ziara hiyo ili kurekebisha maeneo yote.
"Kuongoza ni kuonesha njia sio kufanya jamesisitiza Mhe. Rais Samia na kubainisha
kuwa pale kunapotokea tatizo kati ya pande hizi dawa iwe ni kulitatua badala ya
kuliendeleza.
Kabla ya kuhutubia Bunge, Mhe. Rais Samia amekutana na wafanyabiashara wa Tanzania
na Watanzania waishio Kenya (Dispora) na amewaambia kuwa katika kipindi chake cha
uongozi amedhamiria kukuza uchumi kwa haraka na hivyo ametoa changamoto kwa sekta binafsi kujipanga vizuri kutumia fursa mbalimbali ambazo Serikali ya Awamu ya Sita itazifungua na kuondoa vikwazo mbalimbali
vya biashara.
Ametaja baadhi ya fursa hizo kuwa upanuzi wa huduma za bandari zitakazokidhi mahitaji
na kwendana na kasi ya kukua kwa uchumi, kuanzishwa kwa maeneo maalum ya viwanda
industrial purks yatakayozalisha bidhaa na kuajiri Watanzania wengi, kukuza na kuendeleza kilimo na amewaonya wale ambao wameshikilia maeneo makubwa ya mashamba lakini hawaynendeleza kuwa Serikali itayatwaa maeneo hayo na kuwapatia waliotayari kuzalisha mazao.
"Nataka kwenda faster, nataka kufangua nchi yeyote anayetaka kuwekeza aje awekeze yeye apate na sisi tupate, najina wawekezaji wengi watakuwa wa nje lakini nawaomba na
nyie mchangamke na mtumie vizuri fursa za ndani zitakazozitokez (local content amesisitiza Mhe. Rais Samia, Mhe. Rais Samia ameitaka sekta binafsi ya Tanzania kumtunga mkono katikabdhamira hiyo na amewaomba wafanyabiashara na wawekezaji waliowekeza nje ya Tanzania kurudi kuwekeza Tanzania kwani nyumbani kumenoga. Pia amewataka kuijulisha Serikali pale watakapoona jambo lolote halipo sawa zikiwemo sheria kandamizi ili zifanyiwe kazi.
Mhe. Rais Samia ameagwa na Mhe. Rais Kenyatta na amerejea Jijini Dodoma nchini Tanzania akitokea Jijini Nairobi nchini Kenya baada ya kumaliza Ziara Rasmi ya siku 2
nchini humo.
Post a Comment