MWAKINYO AMCHAPA KWA TKO ANTONIO MAYALA

Bondia wa Kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amempiga kwa TKO, bondia wa Angola Antonio Mayala, usiku wa kuamkia leo katika pambano la ubingwa wa uzito wa Super Welter unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Afrika (ABU).

Mwakinyo ameshinda katika raundi ya 9 kati 12 za pambano hilo lililopewa jina la 'Rumble in Dar II' ambalo lilichezwa Next Door Arena, Masaki jijini Dar es Salaam.

 Hassan Mwakinyo anashikilia rekodi ya kushinda mapambano 18 na kupoteza mawili.

No comments