MUONGOZO WA KUSOMA BIBLIA LEO 28
LESONI, MEI 28
JIFUNZE ZAIDI:
"Ili kufaidi furaha ya kweli yatupasa kusafiri hadi nchi ya mbali sana, na ikibidi hata nje ya sisi wenyewe." —Thomas Browne.
Tazama nukuu hapo juu, iliyoandikwa mnamo miaka ya 1600. Je unakubaliana na kauli hiyo au hapana? Isome kwa muktadha wa #1 Wathesalonike 4:16—18# na #Ufunuo 3:12.#
Augustine aliandika hivi kuhusu hali ya wanadamu: “Haya maisha yetu —iwapo maisha yenye adha tele na magonjwa kiasi hiki bado yaweza kuitwa maisha —hii hutoa ushuhuda kuwa tangu mwanzo, jamii ya wanadamu ni uzao uliohukumiwa. Fikiria, kwanza, shimo kubwa la kutisha la ujinga ambamo ukengeufu wote hutokea na kuwazinga wana wa Adamu katika dimbwi lenye giza ambalo hakuna mtu awezaye kuepuka pasipo jasho, machozi, na hofu.
Kisha, tafakari mapenzi tuliyonayo kwa vitu ambavyo ni sumu na batili kwetu vyenye kutuletea madhara makuu, adha, majonzi, na hofu; wapenda maasi, machafuko, na vita; ukatili na wizi na ujambazi; uhaini na kiburi, wivu na kijicho, wauaji na maharamia, wanyanyasaji na waonevu, waovu na watamanio; tamaa zote mbaya za aibu—waasherati na wazinzi, wabakaji na maovu mengine ya aibu yasiyoweza kutamkika hadharani; uasi dhidi ya dini —kufuru na uzushi, machukizo na ushahidi wa uongo; uovu dhidi ya majirani —wasengenyaji na waongo, walaghai na mashahidi wa uongo, dhuluma kwa watu na mali; upotoshwaji wa haki mahakamani na matatizo mengine yenye kusumbua duniani, ambayo hayajapewa usikivu.” —Augustine of Hippo, City of God, Gerald G. Walsh, S. J. trans. (New York: Doubleday & Co., 1958), book 22, chap. 22, p. 519.
Tatizo hili analolizungumzia Augustine linakabili miji mingi leo ya kisasa; japo imeandikwa zaidi ya miaka 1500 iliyopita. Tabia ya mwanadamu hata hivyo haijabadilika, na hii ndiyo sababu watu wanatafuta ufumbuzi.
Hata hivyo, licha ya mazingira kuwa magumu sasa, siku za usoni ni heri, ila kwa sababu ya kile Mungu alichotenda kwa ajili yetu kupitia maisha, kifo, ufufuo, na huduma ya kikuhani ya Yesu Kristo —iliyo utimilifu wa ahadi ya agano aliloahidiwa Ibrahimu kuwa, katika uzao wake, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Tazama nukuu ya Augustine hapo juu. Andika jambo kwa maneno yako mwenyewe kuelezea hali mbaya inayoukabili ulimwengu leo. Pia tazama aya za Maandiko kile Mungu alichotuahidi kupitia Yesu Kristo (kwa mfano, #Isa. 25:8,# #1 Kor. 2:9,# #Ufu. 22:2—5#). Tafakari ahadi hizo. Zibinafsishe ziwe za kwako. Ni kwa namna hiyo utajua kwa kina maana halisi ya agano.
Post a Comment