MAJALIWA; WATAFITI ONGEZENI KASI YA UBUNIFU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watafiti
na wabunifu nchini kuongeza kasi ya kufanya tafiti ili nchi iende sambamba na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni kote.

Ametoa wito huo Mei 24, 2021 wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dodoma.

"Mabadiliko haya ya teknolojia yanatokea kwa kasi kubwa ulimwenguni yanachochewa na mwenendo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Hivyo basi, nasi hatunabudi kujipanga vyema ili kuendana na kasi hiyo"

Amesema kuwa ni lazima watafiti na wabunifu
katika sekta zote wachukue hatua za makusudi
katika kubuni na kutumia teknolojia zinazoibuka
kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu ya viwanda na jamii yetu.

"Wakati tukifanya hayo yote, ni muhimu pia kujita-
yarisha kutumia kikamilifu matokeo ya tafiti zetu
kama fursa au bidhaa adimu ya biashara
Aliongeza kuwa baada ya tafiti hizo wahakikishe
matokeo ya tafiti yanapelekwa kwa umma ili
uweze kufaidika na matokeo hayo kwa kupata
suluhisho za changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii badala ya kuyafungia makabati.

Aidha, Waziri Mkuu amevitaka vyuo vikuu vyote
nchini kuweka utaratibu wa kufanya utafiti na
kisha kuonesha matokeo ya tafiti ili kusaidia
kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya vyuo na
soko la ajira.

Kadhalika Waziri Mkuu ametoa wito kwa wenye
viwanda kutoa ufadhili wa tafiti na bunifu zinazo-
husiana na bidhaa zinazozalishwa katika viwanda
vyao.

"Tumieni vizuri wataalamu wa vyuo vyetu kwani
wanaweza kuleta majibu ya changamoto mbalim-
bali katika uzalishaji bidhaa, masoko ya bidhaa,
mahitaji ya wateja na mambo mengine mengi"
Pia, Waziri Mkuu amekitaka Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam kutekeleza mpango wa vitengo vya
utafiti kwenye mikoa ikiwemo cha mkoa wa Lindi
ambako tayari walikwisha pewa eneo.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali itaen-
delea kuimarisha tafiti ili taifa liweze kunufaika na
teknolojia ya kisasa na kutoa huduma kwa jamii.





No comments