MAJALIWA; NACTE VISAIDIENI VYUO KUTOA ELIMU THABITI
usimamizi na kuvisaidia vyuo kutoa elimu inayozingatia viwango vya ubora na vyenye kukidhi mahitaji ya soko ya ajira la sasa na lijalo.
Amesema kuwa ni wajibu wa vyuo hivyo kuhakiki-
sha vinatoa elimu bora ili kuwafanya wahitimu
wake wawe mahiri na kukidhi mahitaji ya nchi na
pia kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.
Ametoa agizo hilo (Ijumaa, Mei 28, 2021) wakati
akifungua Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Amesema kuwa vyuo vya elimu na mafunzo ya
ufundi vinapaswa kutumia fursa ya maonesho
hayo kujitathmini na kujipima ili kuona ni kwa
namna gani vinaweza kutoa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi bora yanayokidhi mahitaji ya sasa ya soko
la ajira na kutoa fursa kwa vijana kujiajiri.
"Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025
imeweka wazi kuwa elimu ni kipaumbele cha juu
kwani ndiyo kitovu cha kuleta mabadiliko ya
kiuchumi kwenye jamii".
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ulimwenguni
kote elimu na mafunzo ya ufundi na ufundi stadi
hujulikana kwa mchango wake mkubwa katika
ukuaji wa maendeleo ya viwanda, uchumi na
ustawi wa jamii. "Vyuo na taasisi zinazotoa elimu
hii ni lazima vihakikishe vinatoa elimu bora inayokidhi viwango na mahitaji ya soko la sasa la ajira"
Post a Comment