KENYATTA ALIVYOAGANA NA RAIS SAMIA

Rais Uhuru Kenyatta Jumatano jioni aliagana na mwenzake wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi. 

Rais Samia amerudi nyumbani baada ya kufanikiwa Ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya wakati ambapo alifanya mazungumzo na Rais Kenyatta, alihudhuria Mkutano wa Biashara wa Kenya na Tanzania na kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge kati ya maingiliano mengine rasmi.


No comments