Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesisitiza kwamba uoto wa asili wa mlima kilimanjaro unapaswa kulindwa ili kuufanya mlima huo kuendelea kuwa kivutio kwa watalii wengi wanaokuja hapa nchini.
Jafo ametoa msisitizo huo wakati wa kikao kikufupi na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kigaigai katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Alisisitiza kwamba kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira inaendelea kusimamia uhifadhi wa mazingira hapa nchini kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Naye Mkuu wa Mkoa Mhe. Kigaigai amemuhakikishia Waziri Jafo kwamba atahakikisha juhudi za Serikali za kulinda mazingira anazisimamia ipasavyo katika Mkoa wake.
0 Comments