Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa Manispaa ya Moshi kwa namna wanavyohifadhi taka ngumu zinazozalishwa kila siku katika manispaa hiyo.
Jafo aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya Kikazi katika Manispaa ya Moshi Jana Mei 22, 2021.
Katika ziara hiyo waziri huyo alitembelea dampo la kisasa la manispaa hiyo ambapo alifurahishwa na namna wataalamu wanavyosimamia vyema utupaji wa taka hizo sambamba na ubadilishaji wa baadhi ya taka hizo kuwa mboji.
Jafo amezitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa manispaa hiyo ya Moshi katika uhifadhi bora wa taka ngumu.
Aidha, Jafo pamoja na ukaguzi wa dampo hilo alitembelea kiwanda cha China Paper Industry ambapo aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kutafuta njia ya kutumia nishati mbadala kwani kwa sasa wanatumia magogo mengi kwa ajili ya nishati na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Hivyo amewapa mwaka mmoja wamiliki wa kiwanda hicho kuja na njia nyingine ya nishati mbadala wa magogo yanayotumika sasa.
Pia waziri huyo amewataka wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza nondo cha Five Star Steel kinachotumia chuma chakavu kuepuka kununua vyuma vinavyotoka katika miundombinu ya umma ikwemo madaraja, alama za barabarani na kutoka kwa watu binafsi ili kutoleta hasara kwa jamii.
Hata hivyo, Jafo amekipongeza kiwanda hicho kwa kudhibiti kusambaa kwa moshi kutoka katika kiwanda hicho ambapo kwa siku za nyuma ulikuwa unakera raia wanaoishi jirani ya kiwanda hicho.

0 Comments