Advertisement

Responsive Advertisement

EPSODE 3 NA KANKWI WA KANKWI

Tarehe 31August 2007 siku hii ya ijumaa kulikucha vizuri tu na nikahudhuria vipindi vyangu kama kawaida darasani na mchana wake kulikuwa na Test nikajiandaa nikaenda kufanya vizuri tu sasa baada ya kumaliza nikapokea simu kutoka kwa ndugu yangu akiniomba tukutane mjini na yy anatokea Arusha si unajua mambo ya weekend bana. 

Basi mimi nikatoka darasani nikajiandaa bling bling nikawa nipo sasa nasubiri usafiri nishuke mjini. 

Kule chuoni huwa kuna daladala chache za kusubiria basi wakati nasubiri akaja rafiki yangu mmoja akaniuliza "vipi man leo hatupigi tizi yani mazoezi uwanjani nikamjibu nina kidate mjini kimasihara akanitukana kisha akasema twende uwanjani halafu baadae ntakuitia Tax ije ikuchukue mimi nikamkatalia"akaja mwingine akaniambia kiutani Dogo wakati unasubiri gari twende ukapate moja moto moja baridi 🍻🍻nikacheka nikamjibu nazifata mjini na yy akanitukana baada ya dakika chache ikaja hiace imejaa sana kuna wadada nilikuwa nao wakaniambia dave tupande nikawajibu kimasihara nipande nichafuke gari imejaa hivo siwezi basi wao wakapanda. 

Sasa mbele yangu kulikua na gari Pickup imepaki nikaisogelea nikauliza gari inaenda mjini nikajibiwa ndio dereva yupo wapi nikaoneshwa mshikaji mmoja hivi alikua ni mwanafunzi pia akaniambia panda twende anamsubiri mwenzake basi mm nikapanda akatokea mwalimu wangu akaniuliza wewe leo hufanyi mazoezi nikamjibu hapana nawahi mjini akasema nenda mazoezini ukimaliza mm ntakupeleka mjini kwa gari yangu nikamkatalia na akanionya kwa non verbal yani dereva ame shuka usiende mimi nikajikuta napuuzia. 

Basi jamaa akawasha gari tukaanza safari nakumbuka alikua spidi sana halafu ni mteremko kuna sehem kuna kona kali nikawa naangalia nikipiga hesabu naona kabisa hapigi kona bali anaenda kugonga mbele kulikuwa na nguzo mbili za umeme na mtaro nilichofanya niligonga dirisha lake dereva na kumwambia ANGALIA mbele kuna kona nadhani alistuka na kukata kona kwa nguvu ile gari ikageuka tulikotoka na kutumwaga na mimi nikajirusha kumbe sikuwa najiokoa. 

Baada ya dakika chache nastuka nimelala chini niliokuwa nao kwenye gari ndio nawaona na wengine wananipa pole.

Post a Comment

0 Comments