Wakati nimemaliza sasa A level 2005 nikaanza mchakato wa kutafuta vyuo binafsi nilipenda sana kusomea WILDLIFE na hii hobby nilipenda kwasababu nilivutiwa kiukweli na Kaka yangu ambae kwa sasa ni Marehemu yeye alikuwa kwenye hio field na niliona alifanikiwa mapema sana kimaisha, kuna kipindi nilivyomaliza form 4 ule muda ambao tunasubiri matokeo nilienda kwake Arusha kukaa nae na familia yake nikaona namna alivyofanikiwa na mimi nikapenda sana.
Basi wakati natafuta chuo Baba alitaka sana nisomee Sheria ila mimi sikutaka yani focus yangu ilikuwa niporini na wazungu tu.
Nikaenda Dar kwa ajili ya matriculation ambayo tuliifanya UDSM miaka hio ya 2005 bahati mbaya au nzuri sikupata nafasi.
Sasa usiku nikapokea simu kutoka kwa baba akaniambia ww si unataka wildlife kuna chuo kipo moshi kinaitwa Mweka Wildlife kwahio kesho panda basi hadi moshi ukakitafute,basi nikafanya hivo na kweli nilikipata na nilifurahi sana kwasababu kwanza Chuo ni babkubwa kimazingira na kila kitu na hasa viwanja vya mpira na vifaa vyake basi nikapewa utaratibu nikaambiwa mhula utaanza mwezi wa nane na mm hapo nilifika mwezi wa 7 mwishoni hivi nikaomba nisome short course ya mwezi ili kusubiri mwezi wa 8.
Ikawa hivo ikafika mwezi wa Nane nikaanza rasmi Diploma ya wildlife kiukweli nilikuwa naenjoy sana masomo nilipata marafiki wazuri sana ambao mpaka leo tunawasiliana.
Wakati niko hapo 2007 mwanzoni nilipata fursa moja hivi kwasababu ya Mpira, siku moja tulialikwa kucheza mpira KCMC baada ya pale alinifuata jamaa mmoja hivi akaniomba namba za simu kesho yake alinipigia na kuja chuo tukaonana na akaniomba anipeleke timu ya AFC ARUSHA nikamwambia sasa niko na ratiba ya masomo akaniambia kila weekend niwe naenda Arusha kufanya mazoezi nao basi nikamwelewa akawa kila weekend ananitumia nauli na posho naenda arusha ikiwa nina nafasi basi maisha yakawa yanaendelea Mungu ni mwema.
Sasa buana Tar 31August 2007 ilikuwa siku ya Ijumaa kwenye mida ya saa kumi hivi jioni hii siku ndio kila kitu kilibadilika katika maisha yangu hii siku sitokuja kuisahau maishani mwangu hata ndugu familia na marafiki hawataisahau hii siku.
0 Comments