Advertisement

Responsive Advertisement

EPSODE 1 NA KANKWI WA KANKWI

Miaka 35 iliopita alizaliwa mtoto anaitwa Mcharo lakini baada ya kubatizwa na wazazi wake akapewa jina David huko kilimanjaro kijiji cha Usangi.

Basi makuzi shule msingi mpaka Sekondari alipatia huko kijijini kwao ambapo msingi alisoma shule moja iliokuwa inaitwa Shule ya msingi na Mazoezi Kivindu na kumaliza 1998.

Wakati anamaliza bahati mbaya au nzuri matokeo ya darasa la saba yalifutwa kwa baadhi ya wanafunzi akiwemo David na hii kumpelekea kutochaguliwa shule ya serikali kidato cha kwanza, ila wazazi wangu waliamua kunitafutia shule binafsi na kuanza kidato cha kwanza shule inaitwa LOMWE. 

Nikiwa shule ya msingi nilipendelea sana michezo hasa mpira wa Miguu na hata upande wa shule nikawa kidogo nazembeana hii ilikuwa inawapa shida sana wazazi wangu na mara kwa mara ilikuwa ni kesi kati yangu na wao..sasa baada ya kufanikiwa kuingia sekondari wazazi hawakutaka nisome day scholar waliamua niende bording ili niwe na mda mwingi wa kusoma na kuwa katika uangalizi mzuri, maisha ya bording kiukweli wengi mnafahamu changamoto ni nyingi lakini Niliweza kuyamudu na kufanikiwa kumaliza form 4 mwaka 2002. 

kipindi niko sekondari sikuacha kucheza mpira maana ulikuwa damuni na hata wakati namaliza nilipewa cheti cha mwanamichezo bora. 

Basi bana baada ya kumaliza form 4 matokeo yangu yalikuwa mazuri na hata kuchaguliwa kwenda Alevel Tambaza High school ila sasa baba akanigomea kwenda mjini na kuamua niendelee hapo hapo ALevel maana alihisi mjini lbd ningeharibikiwa nisingesoma.shule ikaendelea hapo mpaka nilipofanikiwa kumaliza Alevel mwaka 2005.

Post a Comment

0 Comments