Basi kuna ile gari iliokuwa imejaza sana ilipofika sehem tupo ikashusha abiria ili inibebe mimi kuniwahisha hospital sasa wakati wana ninyanyua nilikuwa nasikia maumivu mno shingoni nakosa pumzi mwili unakufa ganzi zaidi ikawa hata sijui mguu wa kushoto upo wapi au wa kulia, basi nikapandishwa gari ikanishusha mpaka KCMC.
Kulikuwa na baadhi wa wanachuo walishuka na mm wakachukua simu kupiga kwa ndugu zangu kuwapa taarifa.
Nilipo fika KCMC nikaingizwa emergency room nakumbuka walinichana nguo zangu wakanifunika na shuka then wakanitoa wakanipeleka wodini nikawa nasikia vyumba vimejaa akae hapa kwenye korido hapo niko kwenye stretcher basi usiku baadae wakaja madaktar 3 mmoja raia wa kizungu wapili mchina mwingine mwafrica wakanipa pole kisha wakaniambia nifunge macho kisha kuna ring moja ya chuma wakanivisha kichwani kisha wakaikaza kwa kutumia screw wakamaliza halafu wakaweka mawe huko nyuma yamening'inia ili kusaidia shingo inyooke isilete madhara zaidi.
Basi usiku ukapita asubuhi kukakucha baba na mama na ndugu wengine wakaja kunitazama..Moyoni na akilini mwangu nilikua nawaza vitu vingi sana yani nilikuwa nahisi its Over ujanja kwishaa.
Hapo ndipo maisha yangu yalianza kubadilika nikawa naona giza mbele. Baba na Mama waliumizwa sana mioyo yao ndugu hivyo hivyo.
Nakumbuka baba alikuwa kila akiniangalia.
Nakumbuka baba alikuwa kila akiniangalia.
0 Comments