ASUKILE AFUNGIWA MECHI 5 NA FAINI YA TSH. 500,000/=
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia michezo mitano na faini ya shilingi 500,000 mchezaji wa Tanzania Prisons Benjamin
Asukile.
Kamati ya mashindano ya TFF ilipitia ripoti mbalimbali za michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya kumalizika raundi ya Tano ikiwemo mchezo namba 094 kati ya Tanzania Prisons na
Young Africans.
Kamati imejiridhisha kuwa Asukile ametenda makosa ya kutoa maneno ya kejeli, kashfa, udharilishaji, na shutuma dhidi ya timu pinzani (Young Africans), wachezaji wa kigeni wa Young Africans, Mwamuzi wa mchezo na TFF.
Kufuatia makosa hayo TFF imemfungia kucheza michezo mitano ya mashindano rasmi ya TFF na faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 38:2, 39:5-3 ya kanuni za Ligi Kuu ambazo zinasomeka pamoja na kanuni za Kombe la Shirikisho.
Aidha Kamati kupitia ripoti za mchezo ilibaini Asukile kutoa shutuma za rushwa dhidi ya timu pinzani na shauri hilo limepelekwa katika Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.
TFF inapenda kuwaonya Wachezaji, viongozi na mashabiki kufuata utaratibu wa kanuni za mashindano wanayoshiriki.
Post a Comment