AMKA NA BWANA LEO 8
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumamosi, 07/05/2021.
*KUJIANDAA KWENDA MBINGUNI.*
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? 1Wakorintho 4: 7.
▶️Ni kwamba mwanadamu anaweza kupata uzima ambao ni kipimo cha uzima wa Mungu na kwamba Bwana anavunja miradi yake ya matamanio ya kidunia, ambayo, ikiwa yataruhusiwa kutawala akili, yatamfanya asifae kwa ajili ya ulimwengu ujao.
▶️Mungu anamjaribu kila mmoja wetu. Ametupatia talanta, kuona ikiwa tutakuwa si wabinafsi kabisa katika kuzitumia. Anatuambia waziwazi, “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.” (Luka 16:10). “Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?” (Fungu la 12).
▶️Hebu tukumbuke kwamba tunapaswa kujaribiwa na sheria za ufalme wa Kristo. Sisi hatujimiliki kwamba tunaweza kufanya kama tunavyopenda. Tumenunuliwa kwa bei, na sheria za ufalme wa Kristo, amri kumi takatifu, zinaweka kiwango ambacho kwacho tunapaswa kufikia. Mungu anaonea wivu sheria zake. Anamjaribu kila mwanadamu, kuona ikiwa atatii au la.
▶️Mwanadamu alifanya dhambi na kifo ni adhabu ya dhambi. Kristo aliibeba adhabu hiyo, na alimpatia mwanadamu kipindi cha matazamio. Katika kipindi hiki cha matazamio tunachoishi. Tumepewa fursa ili tujithibitishe kuwa tuna thamani machoni pake Yeye ambaye alimtoa mwanawe wa pekee ili kwamba tusipotee, bali tuwe na uzima wa milele.
▶️Huyu ni Bwana wetu, Kristo. Tunapaswa kukumbuka kwamba sisi ni urithi wake alioununua kwa damu. Mapenzi ya Mungu yanapaswa kuwa mapenzi yetu. Karama za kimwili, kiakili na kiroho tumepewa tuzimiliki. Katika Biblia, mapenzi ya Mungu yamewekwa wazi kwetu. Mungu anamtarajia kila mwanadamu atumie karama zake kwa namna ambayo itampatia maarifa makubwa ya mambo ya Mungu, na kumsaidia kukua, kubadilishwa zaidi na zaidi, kuimarishwa na kusafishwa.
▶️ Katika ulimwengu huu wanaume na wanawake wanapaswa kuzitumia vizuri nafasi zao ili wachukue nafsi miongoni mwa warithi wa mbinguni. Katika dunia hii wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya kubadilishwa kwenda mbinguni. Wale wanaoichukua kazi hii kama Biblia inavyoelekeza, kupitia kwa neema ya Kristo, watakuwa mifano ya kile ambacho watu wote wanapaswa kuwa ambao wanaingia kupitia malango ya jiji lile. —Letter 80, Mei 8, 1903,, kwa Dr. J. H. Kellogg.
*MUNGU AKUBARIKI UWE NA SABATO NJEMA.*
Post a Comment