AMKA NA BWANA LEO 5

KESHA LA ASUBUHI

JUMATANO, MEI, 5, 2021
SOMO: KUONDOKANA NA DHAMBI

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa: bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. 

Mithali 28:13. 



Kwa ajili ya vazi la Babeli na hazina ya dhahabu na fedha, Akani aliridhia kujiuza kwa uovu, na kujiletea katika roho yake laana ya Mungu, kubatilisha cheo chake kwa utajiri wa mali huko Kaanani, na kupoteza matumaini yote ya maisha ya baadaye, urithi wa kutokufa katika dunia mpya.... 



Ugumu na ustahimilivu wake ulikuwa mkubwa sana, kiasi kwamba hatimaye Yoshua alihofu kwamba ataonesha kuwa hana hatia, na hivyo kuibua huruma ya kusanyiko na kuwaongoza kutomtii Mungu. Asingeweza kuungama, kama asingetumaini kuwa kwa kufanya hivyo angeepusha athari ya uhalifu wake. Ni tumaini hili ndilo lililomfanya akiri hatia yake kwa kueleza mambo ya ile dhambi. Kwa namna hii wenye hatia watafanya maungamo watakaposimama katika hukumu na bila matumaini mbele ya Mungu, ambapo kila jambo litakuwa limeamuliwa kwa uzima au kifo. Maungamo yatakayofanywa wakati huo yatakuwa yamechelewa sana kumwokoa mwenye dhambi. 



Kuna Wakristo wengi ambao maungamo yao ya dhambi yanafanana na haya ya Akani. Kwa ujumla, watakiri kutokufaa kwao, lakini wanakataa kukiri dhambi ambazo zinaweka hatia kwenye dhamiri zao, na ambazo zimeleta ghadabu ya Mungu kwa watu Wake. Hivyo wengi wanaficha dhambi za ubinafsi, kutokuwa waaminifu kwa Mungu na kwa jirani yake, dhambi katika familia, na dhambi nyingine nyingi ambazo zinapaswa kukiriwa hadharani. 



Ungamo la kweli linatokana na kuelewa ubaya wa dhambi. Maungamo haya ya jumla si matunda ya mateso ya kweli ya roho mbele ya Mungu. Humwacha mwenye dhambi akiwa na roho ya kubweteka na kuendelea kama alivyokuwa hapo kabla, hadi dhimiri yake inapofanywa kuwa ngumu kabisa, na maonyo ambayo yaligusa nafsi yake hayaonyeshi hisia ya hatari na baada ya muda matendo yake ya dhambi yanaonekana wazi. Atajikuta amechelewa sana wakati ambapo dhambi zake zitamkuta nje, katika siku ile ambapo hakutakuwa na mbadala wa kafara wala sadaka milele. Kuna tofauti kubwa kati ya kukubali ukweli baada ya kuthibitishwa, na kuungama dhambi zinazojulikana kwetu peke yetu na Mungu.



—The Signs of the Times, Mei 5, 1881.

No comments