AMKA NA BWANA LEO 30
KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI, MEI, 30, 2021
SOMO: BILA WAA
Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake ..... apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo, bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Waefeso 5:25—27.
Tunaitwa kwa jina la Mkristo. Hebu tuliakisi jina hili. Kuwa Mkristo humaanisha kuwa kama Kristo. Humaanisha kumfuata Kristo katika kujikana nafsi, kubeba bendera yake ya upendo, kumheshimu kwa maneno na vitendo visivyo vya ubinafsi. Katika maisha ya Mkristo wa kweli hakuna kitu cha ubinafsi, ubinafsi umekufa. Hakukuwa na ubinafsi katika maisha ambayo Kristo aliyaishi katika dunia hii. Akiwa na asili yetu, aliishi maisha ya kujitoa kikamilifu kwa ajili ya mema ya wengine....
Katika neno na vitendo wafuasi wa Kristo wanapaswa kuwa safi na halisi. Katika dunia hii, dunia ya maovu na upotovu, Wakristo wanapaswa kudhihirisha tabia za Kristo. Kwa namna yote ya kufanya na kusema kunapaswa kusiwe na ubinafsi. Kristo anatamani kuwawasilisha kwa Baba “bila ila, wala kunyanzi wala lolote kama hayo,” wakitakaswa kupitia neema yake, wakifanana naye.
Katika upendo wake mkuu, Kristo alijisalimisha kwa ajili yetu. Alijitoa kwa ajili yetu ili kukidhi mahitaji ya roho inayopambana na kuhangaika. Tunapaswa tujisalimishe kwake. Mtu anapojisalimisha kikamilifu, Kristo anaweza kukamilisha kazi ambayo ameianza kwa ajili yetu kwa kujitoa Yeye mwenyewe. Kisha anaweza kutupatia urejeshaji mkamilifu.
Kristo alijitoa Mwenyewe kwa ajili ya ukombozi wa neema, ili kwamba wote wanaomwamini wawe na uzima wa milele. Wale wanaothamini sadaka hii kubwa wanapokea kutoka kwa Mwokozi zawadi ya thamani kuliko zote, moyo safi. Wanapata uzoefu ambao ni wa thamani zaidi kuliko dhahabu na fedha au mawe ya thamani. Wanakaa pamoja katika nyua za mbinguni katika Kristo, wakifurahia katika kuwasiliana Naye furaha na amani ambayo Yeye pekee anaweza kuitoa. Wanampenda kwa moyo na akili na roho na nguvu, wakitambua kwamba wao ni urithi ulionunuliwa kwa damu yake. Utambuzi wao wa kiroho haujahafifishwa na sera za kidunia na matamanio ya kidunia. Wao ni wamoja pamoja na Kristo kwa kuwa yeye ni mmoja na Baba.
Hudhani kwamba Kristo anawathamini wale wanaoishi kikamilifu kwa ajili Yake? Hudhani kwamba anawatembelea wale ambao kama Yohana mpendwa, wapo katika mazingira magumu na yenye majaribu? Anakutana na waaminifu Wake, na anasemezana nao, akiwahimiza na kuwaimarisha.
—The Review and Herald, Mei 30, 1907.
Post a Comment