AMKA NA BWANA LEO 11
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumanne, 11/05/2021.
*NJIA, KWELI, UZIMA.*
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Yohana 15:7.
▶️Kuna watu wengi ambao wanapitiliza usahili wa Yesu Kristo, wakidhani kwamba wanapaswa kufanya kitu fulani kikubwa ili wafanye kazi za Mungu. Mambo ya kitambo yanavutia umakini wa wengine, na wana muda kidogo au kuwazia ukweli wa milele. Wakiwa wamechoshwa na masumbufu ambayo yanaondoa umakini wao kwenye mambo ya kiroho, hawawezi kupata muda wa kuzungumza na Mungu. Daima wanajiuliza swali, ninawezaje kupata muda wa kujifunza na kulitenda Neno la Mungu?
▶️Kristo anajua matatizo yanayoijaribu kila roho, Naye anasema, “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yohana 15:4, 5).
▶️Wajibu wetu wa kwanza na wa juu kabisa ni kujua kwamba tunakaa ndani ya Kristo. Ni lazima Yeye ndiye aifanye kazi. Tunapaswa kutafuta kujua “Kile Anachosema Mungu,” kuyatoa maisha yetu kwa uongozi Wake. Tunapokuwa na Roho ya kukaa kwa Kristo, kila kitu kitabadilika. Mwokozi pekee ndiye anayeweza kutupatia pumziko na amani ambayo tunaihitaji sana. Na katika mwaliko anaotupatia kwamba tumtafute Bwana maadamu anapatikana, anatuita tukae ndani Yake. Huu ni mwaliko, si tu kuja kwake, bali kubaki ndani Yake. Ni Roho wa Mungu ndiye anayetuvuta kuja. Tunapokuwa na pumziko na amani hii, wasiwasi wetu wa kila siku hautatufanya tusienende kwa adabu na bila kujali na kutufanya tusiwe wakarimu. Hatutafuata tena njia zetu na matakwa yetu. Tutataka kufanya mapenzi ya Mungu, kukaa kwa Kristo kama matawi kwenye mzabibu.
▶️Kristo anajitangaza kuwa [Yeye ni] “njia, ukweli na uzima” (sura ya 14:6). Njia ya kwenda mbinguni imewasilishwa kuwa kama ni njia nyembamba, imewekwa kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana kutembea humo. Lakini ukweli unaiangazia njia hii katika kila hatua....
▶️ *Wokovu kwetu humaanisha kusalimisha nafsi, mwili na roho kikamilifu. Kwa sababu ya hali ya ukaidi ya asili yetu hisia zetu mara nyingi ndizo zinatawala. Matumaini pekee kwa mwenye dhambi ni kuacha kufanya dhambi. Kwa njia hiyo nia yake itapatana na mapenzi ya Kristo. Nafsi yake itashirikiana na Mungu.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*.
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment