PART 1. NA MALISA GJ

Niseme kidogo kwa yaliyotokea Dodoma;

Kwa upande wa dogo Shaka nadhani mama hakushauriwa vizuri. Hawezi kuvaa viatu vya Polepole. Katibu mwenezi anapaswa kuwa mtu mwenye maarifa mengi, anayejisomea sana, mwenye uwezo mzuri wa kuongea (fundi wa maneno), mhamasishaji na mwenye kujua kucheza na media, kufanya agenda setting.

Polepole alikua na sifa zote hizi lakini Shaka hana hata moja. Ni mtu aliyepoa, hana maarifa mengi (hata ukimsikiliza utagundua battery low), sijui hata kama anasoma vitabu, hana ushawishi na hajui kufanya agenda setting. Japo anaweza kufundishwa lakini itamchukua muda kuweza kumudu.

Kama ilikua lazima Mwenezi atoke Zanzibar wangetafuta mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko Shaka. Zanzibar ina utajiri wa watu wenye maarifa na uzoefu. Lakini anyway, ngoja tumuone. Akiendelea kula "urojo" tutampa Chaso ajibizane nao. Sisi tutajibu maboss zake 🤣

Kuhusu Katibu Mkuu mpya Godfrey Chongolo , naweza kusema yafuatayo;

1. Ni mtu mwadilifu. Kinondoni ni Halmashauri ya 3 kwa makusanyo makubwa ya kodi baada ya Ilala na Mufindi. Kuna watu walikuwa maDC Kinondoni wakanunua ma-vogue wakaacha hadi kutumia magari ya serikali. Si mnawakumbuka? Lakini kwa Chongolo haikuwa hivyo. Aliishi maisha yake halisi.

2. Hapendi makuu, hajawahi kujimwambafai. Ukimpigia simu hata muda usio wa kazi anapokea. Pia hana kiburi wala majivuno. Kuna wakati amewahi kudhalilishwa hadharani na Makonda lakini wala hakureact. Hizi ni salamu kwa wale viongozi wanaopenda mbwembwe. Wale wanaotembea na mabodyguard kila mahali na kufuatwa na macamera hadi chooni. Waambieni zama zimebadilika, sio kila homa ni malaria.

3. Hakuna mtu aliyedhania wala kuhisi kwamba Chongolo anaweza kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Jina lake lilipotajwa leo kila mmoja ameshikwa na mashangao. Mafanikio ya kwanza katika uongozi ni uwezo wa kudhibiti siri kuvuja.

4. Wale "chawa" walipewa vyeo kwa kumsifia mwendazake na kumuabudu zama zao zimekwisha. Kwa mama hata ujifanye chawa promax kama huna uwezo unatupwa kando. Kuna "chawa gegedu" walianza kumsifu mama bungeni. Tukategemea mmoja wao angepewa ukatibu mkuu. Lakini kawapotezea akamteua Chongolo ambaye si mtu wa kusifu wala kuabudu.

INAENDELEA, SOMA PART 2

No comments