MWILI WA KEZIAH AOKO UMEONDOKA UK KABLA YA MAZISHI NCHINI KENYA

Mwili wa Keziah Aoko Obama, mama wa kambo kwa Rais wa zamani wa Merika Barrack #Obama umeondoka #UK kabla ya mazishi nchini Kenya. Kulingana na vyanzo vya familia, mwili wa Keziah ulitarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kufikia saa sita usiku. Keziah, mama wa Malik, Auma, Aboo na Sadik alifariki katika hospitali ya London mnamo Aprili 13, baada ya kuugua kwa muda mrefu. 

Familia imekuwa ikichangisha fedha kuwezesha kusafiri kwa mwili kwa mazishi nyumbani kwake kwa kijiji cha Kogelo katika Kaunti ya Siaya.

No comments