DKT. MAGEMBE: TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA TIMIZENI WAJIBU WENU


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amezitaka timu za uendeshaji wa huduma za afya katika Mikoa, Wilaya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (RRH) kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ili kupunguza changamoto mbalimbali zinatokea katika sekta ya afya .
Akiongea na Timu hiyo leo Mkoani Tanga

Dkt. Magembe amesema kuwa timu hizo zikitimiza wajibu wao kwa weledi watatua changamoto mbalimbali zinatokea katika Sekta ya Afya hasa katika suala zima la utoaji wa huduma bora za afya, maslahi ya watumishi, uwajibikaji wa watumishi , upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma , kupunguza vifo vya wamama wajawazito na matoto na ukusanyaji wa mapato na matumizi.

Dkt. Magembe anaendelea kufafanua kuwa timu za uendeshaji wa huduma za afya zikitimiza majukumu yao kwa weledi yatasaidia kuimarisha mahusiano bora katika utendajikazi na kuwezesha kutoa huduma bora kwa jamii

Ameesema kuwa wananchi wamekuwa wakitoa malalamiko hasa katika suala zima la utoaji wa huduma bora kwa jamii, timu hizi zina wajibu wa kuhakikisha zinatatua kero kwa haraka na wakati ili kujenga Imani ya wananchi ya kutumia vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Amesema kuwa timu hizo zinawajibu wa kutoa miongozo,, kusimamia maslahi ya watumishi na utendaji kazi wao wa kazi na kuwahimiza kufanyakazi kwa uaminufu na weledi ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuhakikisha inatoa huduma bora za afya kwa jamii.

Dkt. Magembe amuewataka kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya vituo kwenye kamati za afya, menejimenti za halmashauri na secretariat za mikoa.na kuwataka kufunga mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato na kuacha mara moja matumizi ya fedha mbichi

Amesema ufuatiliaji wa kina unatakiwa kufanyika kwa mama wajawazito kwa kuhakikisha wanapitia wodi ya wazazi na kukagua chati ya uchungu, matibabu aliyopewa mama na upatikanaji wa dawa za dharura.

Aidha, ameelekeza taarifa zote za bidhaa za tiba ikiwemo dawa, vitendanishi na vifaa tiba ziwepo, taarifa zionyeshe aina za dawa zilizonunuliwa, matumizi yak

No comments