AMKA NA BWANA LEO 7

KESHA LA ASUBUHI

JUMATANO, APRILI, 7, 2021
SOMO: KRISTO, SUMAKU 

Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. 

Matendo 10:34—35 



Kristo haangalii tabaka wala utaifa. Huichukulia kama haki Yake ya kiungu na isiyoelezeka kufanya kazi kwa uweza na mapenzi Yake, Mkombozi Mwenye huruma alifanya kazi katikati ya matabaka yote, Wakati mtu aliyepooza aliposhushwa kutoka darini mpaka miguuni pake, Alitazama kwa haraka taabu aliyokuwa nayo na punde akatumia nguvu yake kama Mwokozi anayesamehe dhambi kumwambia “Jipe moyo mkuu mwanangu”, “umesamehewa dhambi zako”. (Mathayo 9:2) 



Katika hili baadhi ya waandishi wakaanza kusema mioyoni mwao "Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?" (Marko 2:7) Walishangazwa kiasi gani kuona mawazo yao ambayo hawakuyatamka yamewekwa bayana mbele zao. "Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?" "Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.” ( Mstari wa 8—11). 



Kristo alibadilisha mahusiano ya mdhambi kwa Mungu, akichukua hatia kutoka ndani kabisa. Tajiri mpumbavu alikufa katika utajiri wake mwingi bali mdhambi asiyejiweza aliletwa kwa Kristo, na kwa kuidhihirisha imani yake kuwa Kristo angemponya, hakukatishwa tamaa. Akili yake iliyokuwa haiwezi iliponywa kwanza na kisha Tabibu Mkuu akauponya udhaifu wake wa mwili. 



Ndiyo maana Kristo aliwavuta watu kwake. Alikuwa akifunua kweli ya kiwango cha juu kabisa. Maarifa aliyokuja kuyatoa yalikuwa ni injili tena katika utajiri wake wote na uwezo. Mbeba dhambi, Yu hai katika hofu zote ambazo dhambi huleta nafsini, na alikuja katika ulimwengu huu na ujumbe wa ukombozi. 



Ukristo ni nini? Chombo cha Mungu kwa ajili ya uongofu wa wadhambi. Yesu atamwajibisha kila mmoja ambaye hajaletwa chini ya himaya yake, yeye ambaye hajaonesha mvuto wa msalaba wa Kalvari maishani mwake. Kristo anatakiwa kuinuliwa na wale aliowakomboa kwa kuwafia msalabani. 



—Manuscript 56, April 7, 1899,, “Following Christ.”

No comments