AMKA NA BWANA LEO 30

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 30/04/2021.

*MAAGIZO YA MUNGU.*

*Mwanangu sikiliza maneno yangu; tega sikio lako, usikilize kauli zangu.... Maana ni uhai kwa wale wazipatao, na afya ya mwili wao wote. Mithali 4:20—22.*

▶️Tunaishi katikati ya taabu za siku za mwisho. Roho wa Mungu anaondolewa duniani, lakini Bwana hajakuacha wewe, ndugu yangu. Nimeambiwa nikutie moyo kwamba maisha yako hayajapita bure. Amka, ndugu yangu, na Bwana atakuongoza katika kazi aliyonayo kwa ajili yako. Lakini usimfurahishe tena adui kwa kushindwa majaribu na kukata tamaa. Hebu ukweli wa Mungu uwe katika roho yako kama nuru ya jua na hewa safi. 

▶️Ndugu yangu, je, utaacha kushirikiana na Mponyaji mkuu? Ni muhimu kwamba ufanyie mazoezi misuli yako vile vile neva zako.... Mikono, miguu, viungo vya misuli viliumbwa kwa ajili ya kufanya kazi. Na kama hutavifanyia kazi viungo hivi na uwezo wa akili kwa kadiri inavyofaa, utapoteza nguvu ile ambayo unapaswa kuitunza. 

▶️Bwana amenielekeza nikuambie kwamba unapaswa kutumia viungo vya mwili pia na ubongo. Tafuta kitu ambacho unaweza kufanya katika eneo hilo, na kifanye uweze kutumia nguvu maalumu kwenye miguu pia viungo vya usemi.... 

▶️Ninakumbuka mmoja wa wafanyakazi wetu ambaye miaka kadhaa iliyopita alikuja katika taasisi yetu huko St. Helena. Alikuwa dhaifu sana, alidhani asingeweza kunyanyuka kutoka katika kitanda chake. Daktari iliyekuwa anashughulikia tatizo lake aliniambie, “Sioni tumaini kwake ikiwa hatutamtoa kitandani afanyie mazoezi miguu yake na akili yake kwa namna fulani.” 

▶️Nilimshauri daktari amshawishi mgonjwa huyo ajivishe nguo kwa ajili ya kufanya matembezi mafupi kwa kusudi la kumwomba maoni yake kuhusu kitu fulani. Ilionekana kuwa ni jambo gumu kuamka kutoka kitandani, lakini alifanikiwa, kisha siku iliyofuata, alitembea umbali mrefu kidogo. Baada ya majuma matatu mtu huyu hakuhitaji kusisitizwa zaidi, na baada ya muda mfupi akapata hamu ya chakula cha afya. Hii ilikuwa ni miaka kumi na saba iliyopita, na mtu huyu bado yupo hai, yupo imara kiakili, mifupa na misuli.

▶️ *Ndugu yangu, huwezi kuwa vile unavyopaswa kuwa kimwili kama hutatumia uwezo wa utu wako vile inavyotakiwa.... Bwana ni Msaidizi wako na Mungu wako. Anatamani kulishughulikia suala lako, atashirikiana nawe kadiri unavyotumia kwa usahihi akili, mifupa na misuli. Je, utafuata maelekezo haya ya Daktari mkuu? —Letter 160, Apnili 30, 1907,, kwa Ndugu na Dada J: A. Starr.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏

No comments